Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna dalili za kupungua kwa hewa chafuzi- Ripoti

Bahari inachangia katika kuzuia athari za mabadiliko ya tabianchi kwa kuchukua hewa chafuzi.(Picha:WMO/Olga Khoroshunova)

Hakuna dalili za kupungua kwa hewa chafuzi- Ripoti

Tabianchi na mazingira

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa hii leo imesema viwango vya hewa chafuzi ni vya juu na hakuna dalili yoyote ya mwelekeo huo kupungua.
 

Ikiwa imetolewa na shirika la hali ya hewa duniani, WMO ripoti imetaja hewa hizo kuwa ni pamoja na ile ya ukaa, au hewa ya kaboni, Methani na Nitrasi Oksaidi ambazo viwango vyake vimekuwa vikiongozeka mwaka hadi mwaka.

“Hewa hizo chafuzi zinasababisha mabadiliko ya tabianchi, kuongezeka kwa viwango vya maji baharini, kuongezeka kwa kiwango cha asidi kwenye maji ya bahari na pia hali za hewa za kupindukia, iwe ni joto kali, au baridi kali,” imesema ripoti hiyo ikiwa ni ushahidi zaidi wa athari za mabadiliko ya tabianchi kufuatia ripoti nyingine iliyotolewa na jopo la kiserikali, IPCC,  kuhusu mwelekeo wa tabianchi duniani.

Kama hiyo haitisho, ripoti inasema kuwa kuna ongezeko la hewa chafuzi za CFC-11  zinazosababisha kutoboka kwa zaidi kwa tabaka la ozoni, hewa ambazo zinadhibitiwa na makubaliano ya kimataifa ya kulinda ukanda wa ozoni.

Tathimini mpya kuhusu mabadiliko ya tabianchi iliyofanywa na jopo la kimataifa la Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi IPCC imesema Matumbawe yanaweza kupungua kwa asilimia 70 hadi 90 ikiwa kuongezeka kwa joto duniani kutakuwa kwa 1.5 wakati a
Kadir van Lohuizen/NOOR/UNEP
Tathimini mpya kuhusu mabadiliko ya tabianchi iliyofanywa na jopo la kimataifa la Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi IPCC imesema Matumbawe yanaweza kupungua kwa asilimia 70 hadi 90 ikiwa kuongezeka kwa joto duniani kutakuwa kwa 1.5 wakati ambapo matumbawe zaidi ya asilimia 99 yanaweza kuwa yametoweka yote katika ongezeko la nyuzi joto 2.

Akinukuliwa kwenye ripoti hiyo, Katibu Mkuu wa WMO Petteri Taalas amesema “sayansi iko dhahiri, mabadiliko ya tabianchi yataendelea kuharibu na kuwa na madhara yasiyorekebishika kwa viumbe vya dunia. Fursa ya kuchukua hatua karibu inayoyoma.”

 “Hewa ya ukaa inasalia kwenye anga kwa mamia ya miaka na baharini kwa muda mrefu zaidi. Kwa sasa hakuna mbinu ya kiajabu ya kuondoa hewa yote ya ukaa, au CO2 iliyo angania,” ameonya Elena Maraenkova, Naibu Katibu Mkuu wa WMO akisema kila nyuzi joto ya ongezeko la joto duniani inahusika, na vivyo hivyo kwa kila kiwango kidogo cha hewa zote chafuzi kinachotolewa.
 
Ripoti hii mpya ni nyongeza ya ushahidi unaoongozewa wa athari za joto na hewa chafuzi kwa mazingira kuelekea mkutano wa 24 wa nchi wanachama washirika wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP 24 utakaofanyika kuanzia tarehe 2 hadi 14 mwezi ujao huko Polandi.

Lengo kuu ni kuridhia mpango wa utekelezaji wa mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi uliopitishwa mwaka 2015.

Viwango vya hewa chafuzi vilivyowasilishwa katika ripoti ya leo vinatokana na ufuatiliaji wa viwango vya hewa hizo vinavyotolewa kutokana na shughuli za viwanda, matumizi ya nishati ya kisukuku, kilimo kisichojali  mazingira na ongezeko la ukataji miti kiholela na matumizi  ya ardhi yasiyo endelevu.

Umoja wa Mataifa unataka hatua za dharura ili kupunguza hewa chafuzi na kuhakikisha kuwa viwango vya hewa hizo ni vile vinavyokubalika kimataifa.

Mafuriko katika viunga vya mji mkuu wa Thailand, Bangkok miaka kadhaa iliyopita. Hivi sasa mji huo umebuni namna ya kukusanya maji chini ya ardhi na kuyatumia wakati wa ukame.
ESCAP Photo
Mafuriko katika viunga vya mji mkuu wa Thailand, Bangkok miaka kadhaa iliyopita. Hivi sasa mji huo umebuni namna ya kukusanya maji chini ya ardhi na kuyatumia wakati wa ukame.