Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Itifaki ya Kigali kusongesha mbele biashara- EABC

Meli ya mizigo ikiwa na shehena yake kwenye bandari ya Ningbo, China
IMO
Meli ya mizigo ikiwa na shehena yake kwenye bandari ya Ningbo, China

Itifaki ya Kigali kusongesha mbele biashara- EABC

Ukuaji wa Kiuchumi

Baraza la wafanyabiashara katika jumuiya ya Afrika Mashariki, EABC, limetia shime nchi zote za Afrika kutia saini itifaki ya Kigali inayoruhusu raia wa kutembea huru katika nchi za bara hilo bila vikwazo vyovyote.

Mkurugenzi Mtendaji wa EABC Peter Mathuki amesema hayo huko Kigali, Rwanda katika mahojiano na Priscilla Lecomte wa Umoja wa Mataifa kandoni mwa mkutano wa mwaka wa tume ya uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika, ECA unaoangazia utekelezaji wa mkataba wa eneo huru la biashara barani humo.