Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna nuru katika kuchagiza vijana kujenga stahamala Kenya- Kinaro

Mji Mkuu wa Kenya ambako Shirika la Uzima Foundation lina makao yake..
UN-Habitat/Nathan Kihara
Mji Mkuu wa Kenya ambako Shirika la Uzima Foundation lina makao yake..

Kuna nuru katika kuchagiza vijana kujenga stahamala Kenya- Kinaro

Amani na Usalama

Ukosefu wa ajira kwa vijana ni moja ya changamoto katika kuhakikisha amani katika nchi kwani mara nyingi kundi hili ambalo ni idadi kubwa duniani hivi sasa linatumiwa nabaadhi ya wanasiasa katika kusongesha ajenda zao. 

Hiyo ni kauli ya Bi. Winnie Kinaro Mkurugenzi wa programu katika shirika lisilo la kiserikali la Uzima Foundation lenye makao yake makuu mjini Nairobi, Kenya, kauli ambayo ameitoa wakati wa  mahojiano maalum na Idhaa hii kandoni mwa mkutano wa 8 wa jukwaa la ustaarabu la Umoja wa Mataifa.

Bi Kinaro amesema changamoto hiyo inatokana na…Ametolea  mfano Kenya akisema kazi kubwa ilijitokeza kufuatia vurugu za  zilizotokana na matokeo ya uchaguzi nchini humo mwaka 2007 ambapo kufuatia mafunzo na programu mbali mbali ambazo wanazitoa kwa vijana amesema kuna matokeo chanya.