Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku kubwa kwa watoto kote duniani.

Millie Bobby Brown akiwa mjini New York wakati wa kutengeneza video ya siku ya mtoto mwaka 2018
UNICEF/UN0248272/Clarke
Millie Bobby Brown akiwa mjini New York wakati wa kutengeneza video ya siku ya mtoto mwaka 2018

Leo ni siku kubwa kwa watoto kote duniani.

Masuala ya UM

Wakati dunia ikiadhimisha siku ya mtoto duniani, Millie Bobby Brown ametangazwa kuwa balozi mwema mpya wa Shirika la kuhudumia watoto UNICEF.  Mtoto huyu wa umri wa miaka 14 anakuwa mtu mdogo zaidi kuwa na wadhifa huo wa balozi mwema wa UNICEF. 

 

Akizungumzia uteuzi huo Millie amesema, “Kuwa balozi mwema wa UNICEF ni ndoto ambayo imetimia, ni heshima kubwa kuungana na orodha ya watu ambao wameiunga mkono UNICEF kwa miaka mingi. Ninatazamia kukutana na watoto wengi na vijana wadogo nitakavyoweza, kusikiliza habari zao na kuongea kwa niaba yao” .

Katika majukumu yake haya ya balozi mwema wa UNICEF, nyota huyu wa mfululizo wa maigizo ya filamu ya Stranger Things atatumia nafasi yake kusaidia kukuza ufahamu kuhusu haki za watoto na masuala yenye athari kwa vijana kama ukosefu wa elimu, maeneo salama ya kucheza na kujifunza, matokeo ya vurugu, kuonewa na umaskini. Millie amekuwa akiunga mkono kazi za UNICEF tangu mwaka 2016. Anaungana na orodha ya mabalozi wema wengine akiwemo: Muzoon Almellehan, David Beckham, Orlando Bloom, Jackie Chan, Priyanka Chopra, Danny Glover, Ricky Martin, Lionel Messi, Liam Neeson, Shakira na Lilly Singh.

Akizungungumzia uteuzi huo wa Millie,  Mkurugenzi mkuu wa UNICEF Henrietta Fore anasema, “Ninayo furaha kumkaribisha Milllie katika familia ya UNICEF, hususani katika siku hii ya mtoto duniani-siku ambayo inahusu kumpa mtoto na vijana wadogo sauti. Ninajua kuwa Millie atatumia shauku na kujitolea kwake kulinda haki za watoto na vijana walio katika mazingira hatarishi popote”.


Siku ya mtoto duniani huadhimishwa kila tarehe 20 ya mwezi novemba ili kukuza uelewa na kusongesha haki za msingi za mtoto ambazo ni kuishi, kuendelezwa, kushirikishwa na kulindwa. Miongoni mwa shughuli zinazofanyika katika siki hii ni pmaoja na kuchangia fedha kwa ajili ya watoto ambao hawapati fursa ya shule, hawalindwi na wasio na makazi. 

Katika siku ya leo, UNICEF inawataka watu wote wanaoiunga mkono kupaza sauti zao katika kuwaunga mkono watoto wenye uhitaji. Watu wote wanapaswa kuibadili dunia na kuifanya ya buluu kwa kufanya au kuvaa kitu cha rangi ya buluu iwe shuleni, mitaani, kwenye mitandao ya kijamii, vyumba vya mikutano na katika viwanja vya michezo.

Habari za UN
Kila mtu avae buluu

 

Siyo wanadamu tu, siku hii itaonekana hata katika majengo maarufu  ulimwenguni. Mathalani Sydney Opera nchini Australia, Kituo cha michezo cha kitaifa mjini Beijing China, Petra Jordan, Mnara wa Galata na madaraja kule Uturuki hata jengo la kihistoria katika jiji la New York nchini Marekani yote yatakuwa katika rangi ya buluu.

Watoto 'watatwaa madaraka ya juu ya uongozi'.

Mmoja wa watoto nchi Ireland kwa muda hii leo  ‘atachukua madaraka ya uwaziri mkuu’ wa nchi hiyo. Katika nchi nyingine kama kule Montenegro, Peru, Tonga, Suriname na Zambia, watoto watachukua majukumu ya kibunge. Tanzania Nigeria na kwingine watoto wamo katika vyombo vya habari wakiripoti masuala yanayowagusa wakati kule Brussels vijana wakilitwaa bunge la Ulaya na wakiwaeleza viongozi kuhusu Ulaya wanayoitaka, kule Afrika magharibi na kati vijana watakuwa wakifanya hivyo pia kwa viongozi wao. Leo ni siku kubwa kwa watoto kote duniani.