Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania vyoo bado ni changamoto hasa kwa wasafiri

Watoto wa shule wakienda kujihifadhi chooni katika jitihada za kudumisha usafi. Picha na UM

Tanzania vyoo bado ni changamoto hasa kwa wasafiri

Afya

Katika siku ya choo duniani takwimu zoinaonyesha bado mamilioni ya watu hawana huduma hii ya msingi kote duniani , huku shirika la afya duniani WHO, likitoa wito wa kuhakikisha huduma hiyo inapatikana kwa wote endapo tunataka kutimiza malengo ya afya ifikapo 2030.

Katika kuadhimisha siku ya Choo duniani, kampeni ya mwaka huu ya Umoja wa Mataifa inasema, “asili inapotuita, tunahitaji choo. Lakini mpaka sasa mabilioni ya watu dunani hawana vyoo. Hii ina maana kuwa vinyesi vya binadamu, kwa kiwango kikubwa haviko katika mazingira yanayositahili na hvyo kuchafua maji na udongo ambavyo ni muhimu kwa Maisha ya mwanadamu. 

Lengo la 6 la maendeleo endelevu ni kuhakikisha kila mtu duniani ana choo salama na kuwa kufikia mwaka 2030 hakuna anayemaliza haja zake katika mazingira nje ya choo.

Ili kufahamu hali ilivyo kwa wasafiri wa njia ya barabara nchini Tanzania, John Kabambala wa redio washirika mkoani Morogoro, ametembela kituo cha mabasi cha Morogoro ambacho hupokea mabasi yanayohudumu kote nchini humo na hata katika nchi jirani.