Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sera za Uingereza kuzidisha ufukara kwa masikini:UN

Philip Alston,(kulia) Mtaalm Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu umaskini na haki za binadamu akikutana na Mchungaji mjini Clacton, Uingereza (novemba 2018).
Bassam Khawaja
Philip Alston,(kulia) Mtaalm Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu umaskini na haki za binadamu akikutana na Mchungaji mjini Clacton, Uingereza (novemba 2018).

Sera za Uingereza kuzidisha ufukara kwa masikini:UN

Ukuaji wa Kiuchumi

Sera mpya za  serikali ya Uingereza pamoja na kupunguza  msaada wa kijamii zinachangiakuongezeka kwa kwa kiwango cha umaskini na pia kuleta madhila yasiyohitajika katika moja wa nchi tajiri duniani.

Kauli hiyo imetolewa leo mjini London Uingereza na Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusukupambana na umaskini uliokithiri na haki za binadamu,Philip Alston, baada ya kukamilisha ziara ya kikazi ya siku 12 nchini humo.

Amesema sera hizo zimeleta madhara ambayo hayakuwa ya lazima hususani kwa wafanyakazi masikini , kina mama wanaohangaika kulea watoto peke yao  wakipambana na kila hali , watu wenye ulemavu na mamilioni ya watoto ambao wamewekwa katika kifungo cha mzuznguko wa umasikini ambao wengi wao hawatoweza kuepuka kirahisi.

Bw. Alston ameongeza  kuwa, “hatua ya Uingereza ya kujiondoa kutoka Muungano wa Ulaya ni tishio kwa watu masikini lakini inaonekana serikali haitilii maanani hali hiyo”

Akithibitisha kauli yake amesema karibu uchunguzi wote uliofanywa unaonyesha kama uchumi wa Uingereza utakuwa mbaya zaidi ya ulivyokuwa kabla haijajiondoa kutoka Muungano wa Ulaya. Na athari za mfumuko wa bei, ujira na bei za bidhaa muhimu vitawafanya watu kuwa maskini zaidi ikiwa serikali haitachukua hatua za kuwakinga wale ambao wanapuuzwa na kutumia fungu la sasa kutoka Muungano wa Ulaya kukabiliana na umaskini.

 

 Watu milioni 14 nchini Uingereza sawa na moja ya tano ya watu wote  wanaishi katika hali ya umaskini naasilimia 50 ya watu milioni nne kati yao iwanaishi chini ya mstari wa kiwango cha umasikini kilichowekwa duniani, wakati wengine milioni 1.5 ni mafukara ambao hawawezi kumudu hata mahitaji muhimu yamaisha. 

Baada ya maendeleo sasa umaskini unaingia tena ambapo umaskini miongoni mwa watoto umekisiwa kupanda kwa asilimia 7 kati ya mwaka 2015 hadi 2022. Watu wasio na makazi idadi yao nayoimeongezeka kwa asilimia 60 tangu mwaka wa 2010.

Jambo hilo limemshangaza mtaalam Alston na kusema hii ni fedheha, zahma ya kijamii na mkasa wa kisiasa, vitu vitatu  kutokea katika moja wa nchi tano tajiri duniani.