Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi hususan watoto wasirejeshwa Myanmar iwapo mazingira si mazuri-UNICEF

Zaidi ya nusu ya wakimbizi wa kabila la rohingya huko Cox's Bazar nchini Bangldesh ni wanawake na wasichana.
UNFPA Bangladesh/Naymuzzaman Prince
Zaidi ya nusu ya wakimbizi wa kabila la rohingya huko Cox's Bazar nchini Bangldesh ni wanawake na wasichana.

Wakimbizi hususan watoto wasirejeshwa Myanmar iwapo mazingira si mazuri-UNICEF

Wahamiaji na Wakimbizi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema linasikitishwa na ripoti kuwa wakimbizi wa kabila la rohingya walioko Bangladesh huenda wakarejeshwa kwa nguvu Myanmar na lina hofu kubwa juu ya athari za jambo hilo hususan kwa watoto.

Akizungumza na  waandishi wa habari mjini Geneva Uswisihii leo msemaji wa UNICEF,Christophe Boulierac amesema, “jana wafanaykazi wa UNICEF walioko katika kambi ya Unchiprang Cox’s Bazar walishuhudia idadi kubwa ya wakimbizi warohingya wakiandamana dhidi ya hatua ya kutaka kurudisshwa Myanmar.”

Bwana Boulierac ameongeza kuwa, mamlaka kambinizimesisitiza kuwa licha ya kwamba wako tayari kuwarudisha wakimbizi kwa hiari yao, hakuna mkimbizi warohingya ambaye atalazimishwa kurudi Myanmar bila hiari yake.

UNICEF imesema inakaribisha tangazo hilo la serikali ya Bangladesh na kwamba inakubaliana na mtazamo wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR unaopendekeza kuwa kurejeshwa kwa wakimbizikuwe wa hiari, endelevu na kutekelezwa kwa kuzingatia usalama na utu. Pia UNICEF imesema haitokubaliana na hatua za kuwarejesha watoto ambazo hazikidhi mapendekezo hayo kwani watoto hawapaswi kutenganishwa na watoto au walezi wao au kuwekwa katika hatari yoyote au mtoto mgonjwa kurejeshwa Myanmar.

Msemaji huyo wa UNICEF amesema ripoti kutoka tathmini ya shirika hilo inaonyesha kuwa idadi kubwa ya wakimbizi kambini hawana nia ya kurudi Myanmar hadi pale watahakikishiwa usalama wao.Ameongeza kuwa, “Ni rahisi kuelewa wasiwasi wao, Watoto warohingya na familia walioko jimbo la Rakhine, Myanmar wanaendelewa kukabailiwa na changamoto na wana mahitaji kwa sababu ya kuzuiliwa kutembea na vigumu kwao kupata huduma muhimu za afya na elimu.”

 UNICEF imetoa wito kwa jamii ya kimataifa kuendelea kufanya kazi na serikali na mashirika ya kiraia ya Bangladesh na Myanmar kwa ajili ya watoto na familia za warohingya katika kutafuta suluhu ya muda mrefu kwa ajili ya janga hilo na kulinda haki za warohingya.