Dola milioni 12 zatolewa kunusuru elimu Bangladeshi

14 Novemba 2018

Katika kuitikia changamoto za elimu miongoni mwa jamii ya wakimbizi wa Rohingya nchini Bangladesh, dola milioni 12 zimetolewa kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa matatu ili kuhakikisha kwamba watoto wakimbizi na wenyeji 88,500 wamepata elimu.

Fedha hizo zimetolewa chini ya ufadhili wa ‘Elimu Haiwezi kusubiri’ EWC

Ufadhili huu umetangazwa mapema leo kwneye kituo cha mafunzo ya wakimbizi wa Rohingya wakati wa uzinduzi uliohudhuriwa na wawakilishi 50 wa watoto, wazazi, walimu, serikali, Umoja wa Mataifa na asasi za kiraia.

Fedha hizo zitatumiwa kupitia kwa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF, la Elimu Sayansi an Utamaduni UNESCO na lile la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

Mashirika hayo yatahakikisha kwamba kuna maoni ya pamoja kuhusu uendelevu wa upatikanaji wa elimu bora.

James Lynch, Khaim Mwakilishi wa UNHCR nchini Bangladesh amekaribisha ufadhili huo na kusema ni hatua muhimu wakati huu wa mzozo wa wakimbizi wa Rohingya.

Ameongeza kuwa, elimu ni uwekezaji wa muda mrefu kwani huleta ulinzi wa watoto na kuwa chanzo cha matumaini katika mazingira yasiotabirika.

Edouard Beigbeder ambaye ni Mwakilishi wa UNICEF, Bangladesh amesema wakimbizi wamenyang’anywa haki ya elimu kwa muda mrefu hivyyo ufdhili huu ni mkombozi.

Walimu zaidi ya 2,000 watafaidika na miradi ya kuwapatia ujuzi wa kitaaluma ili kuinua uwezo wao wa kuelimisha, kwa ajili ya kuokoa maisha, kuweka mazingira bora ya elimu msaada wa kisaikolojia kwa watoto na vijana.

Licha ya kwaminika kwamba mchango huu utaleta ahueni, bado wanahitaji dola milioni 60 zaidi ili kukidhi makadirion ya ufadhili wa miradi ya elimu mwaka 2019.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter