Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mataifa yakishikamana, matumaini na suluhusu vinawezekana:Guterres

Katibu Mkuu wa UN akizungumza katika mkutano wa Jukwaa la Amani la Paris Novmba 11-2018
UNESCO/Luis Abad
Katibu Mkuu wa UN akizungumza katika mkutano wa Jukwaa la Amani la Paris Novmba 11-2018

Mataifa yakishikamana, matumaini na suluhusu vinawezekana:Guterres

Amani na Usalama

Kuanzia migogoro, na matatizo ya kiuchumi, hadi maradhi na mabadiliko ya tabia nchi, changamoto hizi za dunia zinahitaji sasa kuliko wakati mwingine wowote mshikamano imara wa kimataifa, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiwaasa viongozi wa dunia kwenye kongamano la kimataifa la Amani lililofanyika leo Jumapili mjini Paris Ufaransa kuadhimisha miaka 100 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema “Katika miaka 100 iliyopita dhamira ya kutokomeza migogoro na vita kwa njia ya amani kwa mantiki ya sheria na misingi ya pamoja imebadilishwa na kuwa mfumo wa kimataifa wa taasisi katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kimazingira.”

Amekumbusha katika taarifa yake ya ufunguzi wa kongamano hilo kwamba “Jinamizi la vita hivyo vikubwa vya kimataifa halitosahaulika , lakini jinamizi halipwaswi kughubika matumaini, kwani ni matumaini kama hayo ndio yaliyoleta kuibuka kwa maendeleo ya ushirikiano wa kimataifa katika karne ya 20” akimaanisha kuundwa kwa jumuiya ya madola mwaka 1919 na Umoja wa Mataifa baada ya vita kuu ya pili ya dunia 1945.

Mtoto mwenye umri wa miezi 18 akiwa amesimama nje ya hema ambamo anaishi na familia yake kwenye kambi ya Saadnayel katika jimbo la Bekaa nchini Lebanon. Vita  nchini mwao vimefurusha maelfu ya watoto.
UNICEF/Romenzi
Mtoto mwenye umri wa miezi 18 akiwa amesimama nje ya hema ambamo anaishi na familia yake kwenye kambi ya Saadnayel katika jimbo la Bekaa nchini Lebanon. Vita nchini mwao vimefurusha maelfu ya watoto.

 

Kongamano hili la Amani la Paris ambalo ni la kwanza la aina yake ni mkakati ulioandaliwa na serikali ya Ufaransa ukiongozwa na Rais Emmanuel Macron. Na limeanza Novemba 11 litakamilika Novemba 13 kwenye mji mkuu wa Ufaransa na kupewa kichwa :”Kongamano la kimataifa kwa ajili ya miradi ya utawala.” Likiwaleta pamoja makumi ya viongozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa kwa ajili ya mijadala mbalimbali na kusisitoza ahadi za kukabiliana na changamoto kubwa zionazoikumba dunia hivi sasa.

“Mazingira ya hofu”

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuna tofauti kubwa iliyokuwepo duniani katika nusu ya kwanza ya karne ya 20 na leo akiongeza kuwa “hii inatupa mazingira ya hofu kwamba matukio yasiyotabirika yanaweza kutokea. Kwa mfano mdororo wa kiuchumi wa mwaka 2008 sawa na ule wa mwaka 1929, ingawa umedhibitiwa na kubadilishwa mwelekeo , asante kwa vyombo na taasisi za fedha , umesababisha kuyumba kwa watu wa kipato cha kati na wengine kuwa tegemezi wa wale wa daraja la juu.

Mfano mwingine alioutoa ni ule wa kuzuka kwa utawala wa kiimla au udikteta miaka ya 1930, ingawa hatuko tena katika zama hizo amesema but tunachokishuhudia hii leo ni ukandamizaji wa maisha ya kisiasa na kijamii ambayo yamesababisha kumomonyoka kwa misingi ya haki za binadamu na uhuru, demokrasia na utawala wa sharia.

Sumu ya Ushirikiano wa Kimataifa

‘Kudhoofu kwa msimamo wa demokrasia na tofauti katika misingi ya pamoja ni sababu mbili ambazo ni sumu ya ushirikiano wa kimataifa amesema Guterres, akisota kidole mgawanyiko ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Syria, ongezeko la mivutano ya kibiashara na changamoto ya kujiamini inayoghubika Muungano wa Ulaya ni baadhi ya mifano.

Familia 400 zimepata hifadhi katika kituo cha makazi ya muda huko Idlib nchini Syria na watoto nao wamepata fursa ya kusomea kwenye mahema
© UNICEF/Aaref Watad
Familia 400 zimepata hifadhi katika kituo cha makazi ya muda huko Idlib nchini Syria na watoto nao wamepata fursa ya kusomea kwenye mahema

 

 

Matokeo dhahiri

Akifafanua kuhusu umuhimu wa ushirikiano wa Kimataifa Katibu Mkuu amesema “umekuwa ni wa lazima, kwani nchi kwa kushirikiana na kufanya kazi pampoja kumezaa matunda yasiyopingika  ikiwemo kupunguza vifo vya watoto wachanga na umasikini uliokithiri katika karne chache zilizopita , kushinda vita vikubwa dhidi ya tishio la afya ya umma kama vile ndui, polio, na ukimwi. Lakini pia mafanikio mengi ya kuzuia vita na juhudi za ujenzi wa amani.

Ameongeza “zaidi ya wanaume na wanawake milioni moja kutoka nchi 125 wamehudumu katika mipango mbalimbali ya ulinzi wa amani katika miaka 70 iliyopita ili kuzuia kusambaa kwa machafuko , kulinda raia na kusaidia mchakato wa kisiasa na kuongezea kwamba operesheni hizo ni za gharama nafuu.

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka China wakielekea Golo, Darfur ya kati kujenga kambi mpya na muda ya UNMID
UNAMID
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka China wakielekea Golo, Darfur ya kati kujenga kambi mpya na muda ya UNMID

 

Pia amesema ushirikiano wa kimataiofa umedhihirisha kuwa unahitajika hasa katika kutatua mgogoro wa uzalishaji wa silaha za nyuklia akitoa mfano wa mshikamano kwenye Baraza la Usalama katika kukabiliana na nyuklia za Iran na hali ya Korea ya Kaskazini au DPRK, uliowezesha majadiliano ya suluhu mar azote 2015 na 2018.