Sri Lanka hakikisheni amani na sheria vinafuatwa:Guterres

10 Novemba 2018

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema anatiwa hofu na hatua ya rais wa Sri Lanka ya kuvunja bunge la taifa hilo na kutangaza uchaguzi mpya  hapo mwakani. 

Katika taarifa iliyotolea leo jumamosi mjini New York Marekani, Bw Antonio Guterres amesema kuwa uamuzi huo wa rais Maithripala Sirisena wa kutaka kufanya uuchaguzi Januari 5 mwaka 2019 kidogo unatia wasiwasi.

Katibu Mkuu amesisitiza umuhimu wa kuheshimu mchakato wa kidemokrasia,  taasisi za serikali na pia kutatua tofauti zao kwa njia ya amani na kufuata sheria.

Guterres pia amerejea wito wake kwa serikali kuhakikisha kuwa amani na usalama kwa raia wote wa Sri Lanka wote vinazingatiwa na pia kuheshimu na kulinda haki za binadamu pamoja na maridhiano.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter