Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Benki ya Dunia yaondoa adha ya jenereta kwa wakazi wa Goree, Senegal

Nyaya za umeme Afrika
World Bank/John Hogg
Nyaya za umeme Afrika

Benki ya Dunia yaondoa adha ya jenereta kwa wakazi wa Goree, Senegal

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Mradi wa Benki ya Dunia wa kutandaza nyaya za umeme baharini, umeondoa adha ya kukatika umeme mara kwa mara iliyokuwa ikikumba wakazi wa kisiwa cha Gorée nchini Senegal. 

Ni mkazi wa kisiwa cha Goree, kilichoko pwani ya Dakar mji mkuu wa Senegal akizungumzia jinsijenereta za umeme zilivyokuwa zinawaletea adha kwani umeme kwa muda mrefu ulikuwa unakatika mara kwa mara.

Augustin Senghor meya wa Goree anafafanua adha hiyo..

Tangu uhuru kisiwa cha Goree kimekuwa kikipata umeme kupitia kebo iliyopitishwa chini  ya bahari.Lakini kutokana na sababu kadhaa kama vile waya kuchakaa na matatizo mengine umeme ulikuwa unakatikakatika.”

Benki ya Dunia ilibaini tatizo hilo katika kisiwa hiki cha Goree ambacho ni eneo la urithi wa dunia na mtaalamu wake Chris Trimble anafafanua..

“Mradi huu umekuwa ukitegemea nishati ya jenereta ambazo zinatumia mafuta kama vile diseli. Lakini sasa tumeweka kebo chini ya baharí ili kuuunganisha Goree na Dakar.”

Kebo hizo zina uwezo wa kuhimili zahma yoyote ndani ya baharí ambapo kupitia video ya Benki ya Dunia wanaonekana wafanyakazi wakihaha kuzifunga na kuzitandaza kwa umakini mkubwa ndani ya maji.

Sasa Benki ya Dunia na shirika la umeme la Senegal, Senelec wanashirikiana kusambaza mita za umeme ambapo wateja wanaweza kununua umeme wakiwa Goree na hata kulipia ankara za umeme kwa kutumia simu za kiganjani na tatizo la umeme ni historia kama anavyoelezea mkazi huyu..

“Hatuna tena umeme wa mgao, wala umeme kuzimika na hali ndio hivyo.”