Skip to main content

Veterani wa vita ya pili ya Dunia. Mtetezi wa wakimbizi.

Harry Leslie Smith mwenye umri wa miaka 95, ambaye ni veterani wa vita ya pili ambaye alishuhudia janga la wakimbizi baada ya vita hiyo.
UNHCR Youtube screen capture
Harry Leslie Smith mwenye umri wa miaka 95, ambaye ni veterani wa vita ya pili ambaye alishuhudia janga la wakimbizi baada ya vita hiyo.

Veterani wa vita ya pili ya Dunia. Mtetezi wa wakimbizi.

Wahamiaji na Wakimbizi

Kutana na Mzee Harry Smith, anayetambulika kuwa muasi mzee kuliko wote duniani. Ni askari mpiganaji  wa vita ya pili ya Dunia. Hivi sasa ni mtetezi wa maslahi ya wakimbizi. 

I am Harry Leslie Smith….

Ni sauti ya mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 95 hivi sasa…alipigana vita ya pili ya dunia na sasa amewekeza nguvu zake kuwatetea wakimbizi

Akiwa mwanajeshi, kijana mdogo katika jeshi la anga la Uingereza, Harry kwa macho yake alishuhudia janga la wakimbizi mwishoni mwa vita ya pili ya Dunia.

“Kulikuwa na msururu wa maelfu ya wakimbizi wakija kusini. Bado ninawaona” anaongea kwa kutetemeka, huku machozi yakimlengalenga.

“Ilikuwa inasikitisha, walikuwa na njaa kali. Ilipowezekana tulisimama na kuwapa chakula chochote cha ziada tulichokuwa nacho katika magari yetu na kuwahakikishia kuwa sasa walikuwa salama”

Hivi sasa Mzee Harry anaishi nchini Canada. Anakutana na wakimbizi kutoka pembe zote za dunia na anawatetea kwa niaba yao, akieleza habari zao kupitia vitabu, magazeti, simulizi na pia ana wafuasi takribani laki mbili katika ukurasa wake wa Twitter.

"Ninafikiri kuna mengi tunaweza kuyafanya ikiwa tutaweka mawazo yetu hapo. Na hatutakiwi kumwacha nje yeyote. Bila kujali utaifa wake, rangi, hali zao” 

Ama kwa hakika penye dhamira hapajali umri.