Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baada ya kusitishwa kwa miaka miwili, IOM yaanza tena safari za ndege Libya

Hii ni mwaka uliopita, 2017, wahamiaji wa Nigeria waliokuwa wamekwama nchini Libya, walipotua Lagos Nigeria kwa msaada wa IOM.
IOM
Hii ni mwaka uliopita, 2017, wahamiaji wa Nigeria waliokuwa wamekwama nchini Libya, walipotua Lagos Nigeria kwa msaada wa IOM.

Baada ya kusitishwa kwa miaka miwili, IOM yaanza tena safari za ndege Libya

Wahamiaji na Wakimbizi

Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM Novemba 8 mwaka huu limeanza tena mpango wa huduma ya hiyari ya safari za ndege za kibinadamu (VHR)  kwa wahamiaji kwenye mji wa kusini mwa Libya wa Sebha.

Huduma hiyo inaotoa msaada kwa wahamiaji waliokwama Libya ambao wanataka kurejea nyumbani kwenye nchi zao kwa hiyari. Katika miezi ya karibuni IOM imepanua wigo wa huduma hiyo katika eneo la Kusini ili kuhakikisha inawafikia wahamiaji wengi Zaidi wanaoihitaji

Ndege ya kwanza ya safari hizo mpya iliyotua mjini Lagos, Nigeria, imefika baada ya majadilino baina ya mamlaka na jamii za Wanaigeria walioko Kusini mwa Libya. Na imefanikiwa kutokana na ushirikiano na ubalozi wa Nigeria mjini Tripoli, na IOM ikawezesha upatikanaji wa pasi za kusafiria za wahamiaji hao kupitia mtandao.

Akifafanua zaidi afisa wa operesheni za mpango huo wa VHR wa IOM , Mohamed Hmouzi amesema “Tumekuwa tukifanya kazi kubwa eneo la Kusini ili kuhakikisha wahamiaji wanaoishi katika mazingira ya mjini au kwenye vituo na wanaotaka kurejea nyumbani salama wanaweza kupata msaada wetu .”

Usafiri wa barabara kwa wahamiaji hao kutoka BraK AL Shati na  Sebha, maeneo yaliyoko mbali kidogo na uwanja wa ndege wa Tamanhent, uliwezeshwa kwa msaada ya uongozi wa maeneo hayo.

Safari hiyo ya kwanza ilibeba wahamiaji 120, wakiwemo wanaume 75, wanawake 30, na watoto wakubwa 6 na watoto wachanga 9. IOM imesema itaendelea kushirikiana na mamlaka za maeneo hayo ili kuhakikisha wahamiaji wote waliokwama Libya wanaohitaji msaada wao kurejea nyumbani wanaupata.