Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pengo la usawa linachochea njaa Amerika ya Kati:FAO/UNICEF/WFP

Wakulima wakipata mlo katika kijiji cha San Lorenzo nchini Mexico. Kijiji hicho kina watu wengi walioikimbia nchi yao ya Guatemala miaka kadhaa iliyopita.
Alex Webb/Magnum Photos for FAO
Wakulima wakipata mlo katika kijiji cha San Lorenzo nchini Mexico. Kijiji hicho kina watu wengi walioikimbia nchi yao ya Guatemala miaka kadhaa iliyopita.

Pengo la usawa linachochea njaa Amerika ya Kati:FAO/UNICEF/WFP

Ukuaji wa Kiuchumi

Njaa, utapiamlo, uhaba wa lishe, pamoja na  utipwatipwa vinaathari kubwa kwa watu wenye kipato kidogo, wanawake, watu wa asili , wale wenye asili ya Kiafrika na pia familia zinazoishi mashambani katika eneo la Amerika ya kati na Caribbean.

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo katika miji ya Santiago de Chile nchini Chile na Panama City nchini Panama.

Ripoti hiyo inasema tangu mwaka 2014 utipwatipwa uliongezeka  kwa idadi ya watu milioni 3.6 kila mwaka katika kanda hiyo huku njaa nayo ikiongezeka katika nchi tatu tangu mwaka wa 2014.

Ripoti hiyo imetolewa na mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa, lile la chakula na kilimo FAO, la kuhudumia watoto la UNICEF,na  la mpango wa chakula la WFP  kwa ushirikiano na shirika la afya  kandaya  Amerika, PAHO.

Ripoti hiyo iitwayo “Changamoto ya uhakika wa chakula na lishe ya mwaka 2018” inamulika  uhusiano kati ya kutokuwa na usawa wa kijamii na kiuchumi unavyochangia  ongezeko la njaa, utipwatipwa na utapiamlo katika watu wengi wa eneo hilo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Amerika ya Kati asilimia 8.4 ya wanawake hawapati chakula cha kutosha wakilinganishwa na asilimia 6.9 ya wanaume huku watu wa asili wakiwa hatarini kutopata chakula kuliko watu wengine

Na katika nchi kumi za ukanda huo, watoto kutoka familia maskini asilimia 20 hudumaa mara tatu zaidi ya familia tajiri, na moja ya sababu kubwa ya kuongezeka utapiamlo ni mabadiliko ya mfumo wa chakula katika eneo hilo na mzunguko mzima kutoka utoka uzalishaji wa chakula hadi matumizi .

Pia imeongeza kuwa utipwatipwa umekuwa tishio kubwa la lishe Amerika ya kati na Caribbean ambapo mtu mmoja wa makamo kati ya wanne ni mnene wa kupindukia. Utipwatipwa unaathiri asilimia 7.3 ya watoto walio chini ya umri wa miaka 5 ambao ni sawa na wtoto milioni 3.9, idadi ambayo inashinda wstani wa idadi ya duniani ya asilimia 5.6.

Ripoti hiyo inasema njaa inawaathiri watu milioni 39.3 ambao ni sawa na asilimia 6.1 ya idadi ya watu wote wa kanda hiyo ya Amerika ya Kati na Caribbean.

Na kati ya mwaka wa 2015 na 2016 idadi ya watu walio kuwa hawapati chakula cha kutosha  ilipanda  kwa idadi ya watu 200,000 na kati ya 2016 na 2017 ilipanda kwa watu 400,000. Hii inaonyesha kuwa kasi ya wasio na chakula cha kutosha inaongezeka.

Venezuela ndiyo taifa lenye  idadi kubwa ya watu wasio na chakula cha kutosha katika kanda hiyo ambao ni watu milioni 3.7 sawa na asilimia 11.7 ya idadi ya watu. Haiti ni ya pili kwa watu milioni 5 sawa na asilimia 45.7 huku Mexico ni ya tatu kwa asilimia 3.8 ya watu.

Pamoja na changamoto hiyo ripoti inasema kuna nuru gizani hasa kwa nchi za Haiti na Mexico kwani kiwango cha njaa kimeanza kupungua katika miaka mitatu iliyopita pamoja n anchi za Colombia na Jamhuri ya Dominica, hizo zikiwa ndiyo nchi nne pekee ambazo zimeweza kupunguza kiwango cha njaa katika ukanda huo tangu mwaka 2014.