Sabuni imenikomboa na kusaidia wakimbizi wenzangu Kakuma :Havyarimana

6 Novemba 2018

Kutana na Innocent Havyarimana, mkimbizi kutoka Burundi anayeishi katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya, ni mjasiriliamali anayetengeneza aina 10 za sababuni na kuziuza kambini hapo kwa wakimbizi wenzie na jamii zinazowahifadhi. Hivi sasa biashara yake inashamiri na kuleta tija kwake, familia yake na wakimbizi wenzie kwa msaada mkubwa wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi , UNHCR. Flora Nducha na taarifa kamili.

Kambini Kakuma, Havyarimana akiwa katika harakati za kutengeneza sabani anazosema alijifunza kupitia mtandao akirambaza kila wakati kupata ujuzi zaidi wa kutengeneza aina mbalimbali za sababuni.

Elimu aliyokuwa nayo ya somo la Kemia kutoka Burundi pia ilimsaidia kwa kiasi fulani na leo hii anapata kiasi cha dola 10 kila siku.

 Bidhaa zake zimeidhinishwa na shirika la viwango nchini Kenya (KEBS).

Mbali ya biashara yake, Kambini Kakuma kuna biashara zisizo rasmi zaidi ya 2100. Je aliwezaje kuanzisha biashara hii?

Hata hivyo shirika la UNHCR limekuwa likiwasaidia wakimbizi hawa kupata vibali vya kufanya biashara kutoka kwa mamlaka ya eneo hilo ambavyo vinaweza kuwasaidia kuanzisha biashara kama anavyofafanua afisa wa UNHCR Kakuma Edith Ingutia

“Vibali vinawapa fursa ya kupata mikopo , na endapo biashara imekua ikiendelea kwa miezi sita, wanafuzu kuomba mikopo, na ni lazima wawe na vibali vya biashara na ni lazima wawe na akaunti ya benki kupata mkopo, hivyo UNHCR kupitia washirika wake inawezesha mchakato huo ili waweze kuendesha biashara zao. Na waweza kupata mkopo kuanzia shilingi 5000 hadi 100,000 za Kenya.”

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter