WFP inaomba Dola milioni 167 kusaidia wathirika wa ghasia CAR
Hali ya usalama Jamhuri ya Afrika ya kati inazidikuwa tete ambapo leo shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP, limetoa wito wa wito jumuiya za kikanda na jamii ya kimataifa kuchukua hatua haraka ili kuzuia kutokea janga la kibinadamu.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini mjini Geneva Uswisi msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP Herve Verhoosel amesema “ WFP ina wasiwasi na hali mbaya ya chakula katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na matukio ya hivi karibuni yanayofanya hali kuwa mbaya zaidi.”
Duru zinasema wiki iliyopita kulitokea machafuko sehemu za Batangafo, kaskazini mwa nchi hiyo kati ya makundi yaliyojihami kwa silaha na kusababishakuchomwa kwa kambi ya wakimbizi wa ndani- IDP- na pia soko na nyumba za karibu na kambi hiyohali ambayo inawaongezea mateso watu wa eneo hilo ambao tayari wanakabiliwa na uhaba wa chakula , makazi pamoja na mahitaji mengine muhimu.
WFP inasema taarifa za awali zinaonyesha kama watu kadhaa waliuawa na wengine kujeruhiwa na watu 27,000 hawana makazi huku 10,000 kati yaowamekimbilia msituni
Kwa mujibu wa WFP, hali katika maeneo mengine kama vile Bambari na Zemio ni ya wasiwasi kutokana na kutokea kwa mapigano kati ya makundi yenye silaha kukabiliana na askari wa MINUSCA na kufanya hali kuwa mbaya zaidi.
Mbali ya hali hiyo WFP na washirika wake wanasema wataendelea na shughulika na utoaji wa misaada kwa wahjitaji lakini ili kukidhi mahitaji hayo takriban dola milioni 167 zinahitajika kuweza ili kukidhi mahitaji hayo kuanzia sasa hadi mwisho wa mwaka wa 2019.