Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi 8 Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika kushikamana mipakani:IOM

Vitengo vya IOM, kile cha ufuatiliaji na uhakiki  na  cha habari kwa umma vilitembelea miradi kadhaa ya IOM katika Puntland, Somalia.
IOM/Mary-Sanyu Osire 2015
Vitengo vya IOM, kile cha ufuatiliaji na uhakiki na cha habari kwa umma vilitembelea miradi kadhaa ya IOM katika Puntland, Somalia.

Nchi 8 Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika kushikamana mipakani:IOM

Wahamiaji na Wakimbizi

Nchi nane za Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika zimeahidi kuanzisha shirika la kiufundi la ushirikiano mipakani litakalowezesha utekelezaji wa masuala 22 yaliyobainiwa kwa lengo la kuboresha ushirika na kuimarisha utendaji wa operesheni za mipakani.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji , IOM, mipaka ya eneo hilo ni miongoni mwa mikapa iliyo na shughuli nyingi kwa sababu ndio njia muhimu ya wahamiaji kutoka kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika lakini pia kuelekea sehemu zingine diuniani ikiwemo Ulaya na nchi za Ghuba.

Shirika hilo linasema kuimarisha ushirikiano mipakani miongoni mwa nchi hizi ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Somalia, Sudan, Sudan Kusini Ethiopia na Djbouti si kazi rahisi lakini baada ya warsha iliyofanyika  mjini Nairobi Kenya na kujumuisha pande zote kuna matumaini.

Warsha hiyo ya kwanza ilitoka na ripoti na mikataba muhimu iliyofikiwa na kuitiwa sahihi na wakurugenzi na maafisa wa uhamiaji kutoka nchi hizo nane chini ya kauli mbiu “mpango wa udhibitio bora wa uhamiaji” (BMM) mpango huo wa muda mrefu unafadhiliwa na wakfu wa Muungano wa Ulaya kwa ajili ya Afrika na wizara ya ushirikiano wa koiuchumi na maendeleo ya Ujeriuamani.

Kwa mara ya kwanza miongoni mwa mikataba iliyowekwa saini ni baina ya Ethiopia na Sudan kusini kufanya doria ya pamoja na kushirikiana kufungua kituo kipya cha uhamiaji baina ya nchi hizo mbili, Sudan na Sudan Kusini walitia saini kufanya kazi pamoja kufungua vituo vinne vya ukaguzi mipakani mwao kikiwemo kituo kikubwa kimoja cha pamoja.
Uganda na Sudan Kusini wameafikiana kuanzisha na kutekeleza ushirika wa doria mipakani na kuzindua kamati za udhibiti wa miaka .

Kwa upande wa Tanzania, Somalia na Kenya wamekubaliana kutekeleza mpango wa kamati za pamoja za udhibiti mipakani na kuwa na shirika la pamoja, vilevile kufanya doria mipakani.

Wakati Ethiopia, Kenya na Tanzania wameafikiana kuongeza ushirikiano na utekelezaji wa masuala mazuri muhimu katika kupambana na usafirishaji haramu, na kufanya doria za pamoja mipakani.