Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Akiwa Jordan, Griffiths akutana na wawakilishi wa jamii za Yemen

Martin Griffiths,Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mzozo wa Yemen.
UN Geneva/Violaine Martin
Martin Griffiths,Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mzozo wa Yemen.

Akiwa Jordan, Griffiths akutana na wawakilishi wa jamii za Yemen

Amani na Usalama

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Yemen Martin Griffiths, amekuwa na mkutano wa mashauriano na kundi la watu huru linalowakilisha idadi kubwa ya wakazi wa nchi hiyo.

Mazungumzo hayo yamefanyika Amman, Jordan ikwa ni ya pili kuleta pamoja watu mbalimbali Yemen wenye mtazamo usioegemea pande zinazokinzana Yemen.

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa wa Umoja wa Mataifa hii leo mjini New York, Marekani imesema Bwana Griffiths na watu hao wamejadili hali ya sasa ya Yemen na harakati zake za kurejesha mchakato wa siasa.

“Zaidi ya asilimia 30 ya washiriki wa mashauriano hayo walikuwa wanawake ambapo walijadili masuala mbalimbali ikiwemo kuzorota kwa hali ya kiuchumi na kibinadamu Yemen, ukosefu wa huduma za msingi pamoja na kile ambacho kinapaswa kufanyika ili kudhibiti mzozo wa Yemen,” imesema taarifa hiyo.

Mkutano wa kwanza wa aina hii uliofanyika London, Uingereza mwezi Agosti mwaka huu.