Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati wa kuchukua hatua Yemeni ni sasa: Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiongea na wanahabari (Maktaba)
UN /Mark Garten
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiongea na wanahabari (Maktaba)

Wakati wa kuchukua hatua Yemeni ni sasa: Guterres

Amani na Usalama

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo akiwa katika katika makao makuu ya Umoja huo mjini New York Marekani, amesema kinachoendelea nchini Yemeni siyo janga la asili bali ni janga linalosababishwa na binadamu.

Guterres amesema Yemeni inaning’inia ukingoni kutumbukia katika zahma kubwa kabisa ya kibinadamu na hali ni ya kusikitisha. Na kuongeza kuwa

“Tunatakiwa wote kufanya kila tuwezalo  kuzuia hali mbaya iliyopo sasa ili isiendelee kuelekea kuwa baa baya zaidi la njaa kuwahi kutokea katika miongo kadhaa”

Amesema jumuiya ya kimataifa ina fursa ya kusitisha mzunguko wa vurugu na kuzuia janga linaalokaaribia kutokea kwani “Wakati wa kuchukua hatua ni sasa”.

Aidha Guterres ameongeza kuwa kwa miezi kadhaa kuongezeka kwa mapigano ya kijeshi na kusambaratika kwa uchumi vimeifanya hali iliyokuwa mbayaa kuwa mbaya zaidi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pia amekumbushia kuwa wiki iliyopita, mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na usaidizi wa dharura, OCHA, Mark Lowcock, alilitahadharisha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa Yemeni ilikuwa karibu na baa la njaa kuliko wakati mwingine wowote.

Umoja wa Mataifa na washirika wake tayari wanawalisha watu milioni 8 wa Yemen. Bila hatua za haraka, kufikia watu milioni 14, nusu ya idadi ya watu wote wa Yemen, wanaweza kuwa katika hatari ya katika miezi ijayo” amesema Guterres.

Vijana wa kiume wakiwa wamesimama katika jengo lililobomolewa sehemu za Saada Yemen. Mkuu wa OCHA asema nchi hiyo inakaribia kutumbukia katika baa la njaa ikiwa msaada hautatolewa haraka.
WFP/Jonathan Dumont
Vijana wa kiume wakiwa wamesimama katika jengo lililobomolewa sehemu za Saada Yemen. Mkuu wa OCHA asema nchi hiyo inakaribia kutumbukia katika baa la njaa ikiwa msaada hautatolewa haraka.

 

Bwana Guterres pia ametoa ushauri wa kile kinachotakiwa kufanyika ili kuinusuru Yemeni akisema, kwanza ni kusitisha vurugu kila mahali, pili vyakula kwa ajili ya kuwasaidia watu, nishati na mahitaji mengine yanatakiwa kuruhusiwa kuingia Yemen bila vikwazo, pia barabara zinatakiwa kubaki wazi ili bidhaa kwa ajili ya uokozi wa maisha ziweze kuzifikia jamii nchini kote na kila mahali, tatu uchumi wa Yemeni unatakiwa kusaidiwa. Hii ni pamoja na kuchukua hatua muhimu kuimarisha viwango vya ubadilishaji fedha, kulipa mishahara na viinua migongo, nne, misaada ya kifedha ya kimataifa inatakiwa kuongezeka hivi sasa ili mashirikOCHAa ya misaada ya kibinadamu iweze kuongeza huduma zake muhimu.

Na kwa upande wa Yemeni yenyewe, Guterres amezitaka pande zote mbili kushirikiana na Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchni Yemeni Martin Griffiths katika kuumaliza mgogoro.

Sote tunatakiwa kufanya kila tuwezalo kumaliza mateso kwa wanadamu na kuepuka janga baya lisifikie kuwa baya zaidi” amesisitiza Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.”