Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirika katika utafiti wahitajika kupambana na viwavi jeshi Afrika :FAO

Viwavijeshi kwenye mashamba kusini mwa Afrika. Picha: FAO

Ushirika katika utafiti wahitajika kupambana na viwavi jeshi Afrika :FAO

Tabianchi na mazingira

Wajumbe wanaohudhuria mkutano wa kwanza wa kimataifa kuhusu utafiti wa viwavi jeshi kwa ajili ya wamendeleo wametoa wito wa kuwepo uratibu na utafiti imara katika juhudi za kupambana wadudu wa aina mbalimbali wanaoshambulia mazao.

Mkutano huo unaofanyika mjini Addis Ababa Ethiopia umeandaliwa na wadau mbalimbali ikiwemo Tume ya Muungano wa Afrika, Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO, CABI, IITA na shirika la Marekani la msaada wa maendeleo ,USAID.

 

Viwavi jeshi vikishambulia mmea wa mahindi Lesotho
FAO/Lesotho/Lechoko Noko
Viwavi jeshi vikishambulia mmea wa mahindi Lesotho

Bi. Amira Elfadil, kamishina wa masuala ya kijamii wa Muungano wa Afrika AU, amewakumbusha wajumbe kwamba Africa inahamasa kubwa ya kujikita katika ushirika wa kimataifa ambao unatoa fursa ya ushirikiano endelevu wa utafiti ,mabadiliko na kujifunza ili kuwezxa kudhibiti vyema viwavijeshi katika kila kona barani Afrika.Ameongeza kuwa “Nimeridhika kwamba katika mkutano huu , kazi yenye hamasa ya kuanzisha mpango wa utafiti wa maendeleo kwa kutumia vifaa vyenye ushahidi kuwa ni salama , vizuri , vinavyoweza kupatikana na endelevu vinatengenezwa na kuletwa barani  Afrika.

Ameongeza kuwa licha ya juhudi za kudhibiti viwavi jeshi wadudu hao wanaendelea kushambulia katika maeneo mengine. Hivi karibuni wamebainika nchini India kwa mara ya kwanza na kuonyesha ni jinsi gani wanaweza kusafiri mbali kwa muda mfupi.

Amehimiza kuwa juhudi za pamoja na rasilimali vinahitajika ili kuweza kuwa na suluhu endelevu ya kukabiliana na wadudu hao lakini pia kuokoa mabilioni ya dola ambayo ni hasara ya kila mwaka ya upotevu wa chakula katika nchi nnyingi za Afrika.

 

Mkulima katika shamba lake lililoshambuliwa na viwavi jeshi huko Namibia
FAO/Rachael Nandalenga
Mkulima katika shamba lake lililoshambuliwa na viwavi jeshi huko Namibia

Wakulima kuwa mstari wa mbele katika vita hivi

Mkurugenzi wa Faidara ya upandaji na ulinzi wa mazao Hans Dreyer amesema “Hakuna suluhu moja pekee itakayodhibiti kikamilifu viwavi jeshi na hivyo , hata hivyo hatuhitaji kubuni mbinu mpya bali tunahitaji ushirikiano , kuna utalaam mwingi tayari na ujuzi ukiwemo wa asili katika bara la Afrika na kwingineko lakini mkulima lazima awe ndio kitovu katika juhudi zetu.”

Ameongeza kuwa wakulima wadogowadogo barani afrika wanaendelea kubeba gharama kubwa za athari za viwavijeshi katika mahsmaba yao ya mahindi, na pia mtama na ulezi hivyo ni muhimu kufikiria jinsi ya kudhibiti na hatua za kuchukua kwa mtazamo wa wakulima.

Viwavijeshi vyashambulia nyasi barani Afrika.
FAO/Lesotho/Lechoko Noko
Viwavijeshi vyashambulia nyasi barani Afrika.

 

Kwa miaka miwili iliyopita Fao imeendesha miradi mbalimbali Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kusaidia wakulima na serikali kukabili athari za viwavijeshi, ikiwemo kutumia teknolojia , kufuatilia, na kuweka mifumo ya tahadhari za mapema , ikiwa ni pamoja na mwongozo kwa ajili ya wakulima na wafanyakazi wa serikali wa jinsi gani ya kuddhibiti wadudu hao.

FAO imetekeleza zaidi ya miaradi 40 iliyogharimu dola milioni 12 ya kupambana na wadudu barani Afrika kwa msaada wa wafadhili kama Bank ya Afrika, serikali ya Ubelgiji, Ireland, Japan, Norway na USAID-OFDA.

 

App (programu tumizi) mpya inayoongea, inawasaidia wakulima kama Tazelekwew, kusini mwa Ethiopia kufahamu kama mazao yao yameathiriwa na wadudu.
FAO/Tamiru Legesse
App (programu tumizi) mpya inayoongea, inawasaidia wakulima kama Tazelekwew, kusini mwa Ethiopia kufahamu kama mazao yao yameathiriwa na wadudu.

Muungano mmpya wa utafiti

Mashirika 35 yameshikamana na kuweka juhudi zao pamoja katika muungano wa kimataifa wa utafiti kwa ajili ya maendeleo ili kuanzisha msingi wa kisayansi ambao ni wa lazima kwa ajili ya udhibiti endelevu wa viwavijeshi.

Kwa mujibu wa juhudi hizo zinazoongozwa na FAO za kukusanya utaalam unaotakiwa kushughulikia changamoto ya viwavijeshi , kazi hii itaimarishwa na uratibu wa mfumo wa utafiti ambapo muungano huo utatoa fursa mpya kubaini na kutoa kipaumbele katika masuala ya kuyafanyia utafiti kwa ajili ya maendeleo ya kupambana na viwavijeshi.