Watoto 9 kati ya 10 huvuta hewa chafu kila siku kote duniani: WHO

29 Oktoba 2018

 Zaidi ya asilimia 90 ya watoto duniani kote  walio na umri  wa chini ya miaka 15 huvuta  hewa chafu kila siku ambayo inaweka maisha yao hatarini na wengi wao hufariki dunia imesema ripoti ya shirika la afya dunaini WHO.

Ripoti hiyo mpya  ya WHO iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi, inasema  kila siku watoto bilioni 1.8  walio katika umri wa chini ya miaka 15 wanavuta hewa chafu ikiwa ni sawa na asilimia 93 ya watoto wote , na WHO inakadiria kuwa mwaka wa 2016  pekee watoto 600,000 walifariki dunia kutokana  mifumo yao  ya kupumua kuathiriwa na hewa chafu.

 Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt Tedros Adhanom Ghereyesus, hali hii haivumiliki kwani kila mtoto ana haki ya kuvuta  hewa safi ili aweze kukua na kufikia uwezo wake katima maisha.

Ripoti hiyo kuhusu " uchafuzi wa hewa na afya ya mtoto" imezinduliwa katika mkesha wa mkutano wa kwanza kuhusu uchafuzi wa hewa na afya kuwahi kufanywa na WHO.

 Mkurugenzi wa idara ya afya ya umma, mazingira na jamii wa shirika hilo , Dkt Maria Neira  amesema hewa chafu inasababisha ubongo wa mtoto kudumaa na  kuna  njia nyingi za kusaidia kukabiliana na hewa hiyo chafuzi kwani 

Jion, wazazi na watoto wakivuka barabara wakati wanatoka shuleni ewilayani Songinokhairkhan Ulaanbaatar, Mongolia ambako uchaguzi wa hewa ni wa kiwango cha juu mjini humo.
Picha na © UNICEF/Mungunkhishig Batbaatar
Jion, wazazi na watoto wakivuka barabara wakati wanatoka shuleni ewilayani Songinokhairkhan Ulaanbaatar, Mongolia ambako uchaguzi wa hewa ni wa kiwango cha juu mjini humo.

(SAUTI YA DKT MARIA NEIRA)

“  Wasiwasi wetu ni kuwa   itasababisha madhara kwa mishipa ya fahamu na kufanya kiwango cha ufahamu wa mtoto kuwa chini  katika kutambua mambo. lingine tunalojua ni kwamba uvutaji wa hewa chafu unauwezekano wa kusababisha ugonjwa wa pumu na ikiwa tayari unayo pumu basi hufanya hali kuwa mbaya zaidi.”

 Amsema WHO inaunga mkono hatua za kisera kama vile kuharakisha hatua za kutumia nishati mbadala kwa ajili ya kupikia ,  usafiri usiochafua mazingira  pamoja na nyumba zinazojali mazingira.

 Ripoti imetaja  athari nyingine za hewa chafu kwa mfano mama mjamzito akivuta hewa hiyo anaweza kujifungua  mtoto kabla ya wakati au njiti na mtoto kuwa na uzito mdogo sana. Pia ripoti inaendelea kuainisha kuwa hewa chafu inaathiri neva na  inaweza kusababisha ugonjwa wa pumu na saratani ya utotoni.

Vilevile watoto ambao wameathirika kwa kiasi kikubwa na hewa hiyo chafu  wako hatarini kupata magonjwa kama vile ya moyo katika maisha yao ya baadae.

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter