Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu 11 wauawa wakiwa kwenye ibada, Katibu Mkuu wa UN akemea vikali.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres
UN Photo/Mark Garten)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres

Watu 11 wauawa wakiwa kwenye ibada, Katibu Mkuu wa UN akemea vikali.

Haki za binadamu

Nchini Marekani katika mji wa Pittsburg jimboni Pennsylvania, watu 11 wameripotiwa kuuawa na mtu mmoja aliyekuwa na silaha wakati watu hao wakiwa kwenye ibada.

Tukio hilo la Jumamosi limetokea katika sinagogi moja la wayahudi ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikalo shambulio hilo.

Kupitia msemaji wake, Beana, Guterres ametuma salamu za rambirambi kwa wafiwa akitakia ahueni ya haraka majeruhi.

Amesema shambulio hilo mjini Pittsburg ni kumbukizi ya majonzi ya mwendelezo wa chuki dhidi ya wayahudi.

Bwana Guterres amesema “wayahudi kote duniani wanaendelea kushambuliwa kwa sababu ya utambulisho wao."

Amesema chuki ya ugaidi ni jambo linalokwamisha maadili ya demokrasia na amani na ni haipaswi kuwa na nafasi katika karne ya sasa ya 21.

Bwana Guterres ametoa wito wa kuungana kwa pande zote ili kuondokana na vitendo hivyo vya chuki dhidi ya wayahudi, uislamu na aina zote za ubaguzi na chuki dhidi ya wageni, vitendo ambavyo amesema vinashamiri maeneo mengi duniani.