Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mauaji haya ya kinyama na utekaji DRC lazima vikome:Guterres

Mtoto wa miaka 7 akiwa shuleni Ndindi kiunga cha Beni mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. watoto kama huyo wako katika hali tete, mbali na Ebola pia wanasumbuliwa na makundi ya wapiganaji.
© UNICEF/Thomas Nybo

Amani na Usalama

Nimeghadhibishwa na kuendelea kwa mauaji na utekaji wa raia unaofanywa na makundi yenye silaha mjini Ben katika jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres , kupitia taarifa iliyotolewa leo na msemaji wake, akilaani vikali mauaji ya raia 11 akiwemo mtoto mmoja  wa kiume, watu wengine kujeruhiwa pamoja na watoto kadhaa kutekwa wakati wa shambulio lililotokea kwenye mji wa Mayongose nje kidogo ya eneo la Beni.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa , Katibu Mkuu pia amesikitishwa na tarifa kwamba Ijumaa ya 19 Oktoba maafisa wawili wa afya raia wa DRC waliokuwa wakisaidia kupambana na mlipuko wa Ebola waliuawa kwenye eneo la Butembo wakati wanamgambo wenye silaha waliposhambulia kitengo cha jeshi la Congo .

Guterres ametoa wito kwa makundi yote kusitisha uhasama mara moja dhidi ya raia na kuhakikisha fursa ya kufikisha misaada ya kibinadamu kwenye maeneo inayohitajika.

Amerejelea kuwaambia watu wa DRC kuwa Umoja wa Mataifa unashikamana nao hususan kwenye maeneo yaliyoathirika na Ebola vita.