Wataalam wa takwimu wakutana kusaka suluhu za changamoto zinazoikabili dunia:    

Kongamano la Umoja wa Mataifa la takwimu Duniani
Nembo na UN/World Data Forum
Kongamano la Umoja wa Mataifa la takwimu Duniani

Wataalam wa takwimu wakutana kusaka suluhu za changamoto zinazoikabili dunia:    

Wahamiaji na Wakimbizi

Wataalam wa kimataifa wa takwimu kutoka ofisi za kitaifa, sekta binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali yaani NGO’s, wanazuoni, na mashirika ya kimataifa na kikanda, wamekusanyika mjini Dudai katika Falme za Kiarabu kuanzia leo katka jitihada za kusongesha mbele mchakato wa kutimiza malengo ya maendeleo endelevu au SDG’s.

Katika mkutano huo wa Umoja wa Mataifa wa siku tatu utakaokunja jamvi Jumatano wiki hii, wataalam hao watazindua suluhu bunifu ya kuboresha takwimu za wahamiaji, masuala ya afya, jinsia na maeneo mengine muhimu kwa ajili ya maendeleo endelevu .


Mkutano huo wa pili wa kila mwaka utakuwa na matukio na vikao takribani 80 na unaonekana kuwa ni fursa nzuri kwa wazalishaji na watumiaji wa takiwmu katika kusaka njia bora za kuto takwimu kwa watunga sera  na raia katika nyanja zote za SDG’s.


Akizungumza kabla ya ufunguzi wa mkutano huo Liu Zhenmin, mwakilishi wa Katibu Mkuu kwa ajili ya masuala kiuchumi na kijamii amesisitiza umuhimu wa takwimu katika kufikia SDG’s

(SAUTI YA LIU ZHENMIN)
“ Ni muhimu kuwa na tamwimu sahihihi, za kuaminika, kwa wakati na zilizokusanywa pamoja kwa ajili ya kufuatilia masuala ya kiuchumi, kijamii na malengo ya mazingira katika ajenda ya 2030. Katika kongamano la Umoja wa Mataifa la takwimu natarajia kuundwa kwa ushirika mpya, kutangazwa kwa ahadi na kuongezwa kwa msaada.”

Mkutano huo unafanyika miezi miwli kabla ya kupitishwa na nchi wanachama mkataba wa kimataifa wa uhamiaji , ambao utakuwa mkataba wa kwanza kabisa  wa Umoja wa Mataifa duniani ulio na lengo la pamoja kuhusu uhamiaji wa kimataifa.

Namoja ya vikao vya ngazi ya juu katika kongamano hili itakuwa ni kuboresha takwimu za uhamiaji ili kusaidia kuweka mikakati mipya ya jinsi gani ya kufuatilia vyema takriban wahamiaji zaidi ya milioni 258 kote duniani , ikiwa ni pamoja na vyanzo vya takwimu za wakati huohuo kama vile kumbukumbu za simu. Na huu utakuwa ni mchango katika mkutano wa Desemba wa uhamiaji.

Miongoni mwa mada kuu zitakazopewa kipaumbele na kongamano hilo ni ufadhili kwa ajili ya takwimu na kumbukumbu na njia za kuziba pengo la ufadhili na takwimu zilizopo katika nchi nyingi .

Mada hiyo itajadiliwa katika wakati ambao nchi zinazoendelea zinakabiliwa na pengo la dola milioni 200 kwa mwaka na zaidi ya nchi 100 hazina takwimu kamili za uandikishjaji wa vizazi na vifo, huku ukata na uwezi vikiwa ndio vbizingiti vikubwa kwa nchi nyingi.


Mada zingine zitakazoangaziwa na kongamano hilo ni pamoja na haja ya kuwa na takwimu za wazi, kuwezesha kushirikiana takwimu na ujumuishwaji wa vyanzo vipya vya takimu katika kumbukumbu rasmi.