Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Teknolojia mpya isifunike vyombo vya habari asilia:Wajumbe

UN Photo/Pierre-Michel Virot
Balozi Modest Mero, mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa

Teknolojia mpya isifunike vyombo vya habari asilia:Wajumbe

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Kukataa kuzigeuza habari za umma kuwa siasa, au kulinda waandishi wa habari, si kupuuza vyombo vya habari vya jadi, na kugeukia mtandao wa inteneti na mitandao ya kijamii.

Wito huo umetolewa na wajumbe mbalimbali kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa katika mkutano wa mwishoni mwa wiki wa Kamati ya Nne ya mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa uliojikita katika masuala ya habari.


Wajumbe pia walijadili kazi za idara ya habari ya Umoja wa Mataifa, ikiwemo kuunga mkono mabadiliko ya idara hiyo yaliyostahili kufanyika muda mrefu uliopita.


Kwa mujibu wa mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Modest Mero mabadiliko hayo yataruhusu Umoja wa Mataifa kufikisha taarifa kwa watu kupitia lugha wanazozielewa na katika njia mbalimbali lakini akihimiza kuwa mawasiliano kupitia njia za jadi kama radio bado ni kiungo muhimu hususan kwa jamii za mamilioni ya watu katika nchi zinazoendelea.

Ameongeza kuwa njia za kisasa za technolojia ya kidijital pia zina mchango katika kutimiza lengo hilo japo si mkubwa kama ule wa njia za jadi kwa baadhi ya mataifa hususan Afrika.


Hoja hiyo iliungwa mkono na mwakilishi wa kudumu wa Ukraine kwenye Umoja wa Mataifa , Oleg Nikolenko ambaye kwa upande wake alitilia mkazo njia zamawasiliano za kidijital.


Suala la kutumia lugha, mbalimbali katika kufikisha ujumbe kwa umma kuhusu kazi za Umoja wa Mataifa limeungwa mkono na mjumbe wa Urusi ambaye alitoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuwa “Msitegemee tu wanaozungumza kiingereza”.

Balozi huyo pia ametathimini mafanikio ya idara hiyo kwa kutumia njia mpya za mawasiliano na kusema kuwa bado ni “muhimu kuendelea kutoa uzito unaostahili na kushirikiana na vyomboa vya jadi vya mawasiliano kama Radio na televisheni” hoja ambayo iliungwa mkono kwa kiasi kikubwa na wawakilishi wa Cuba na Tanzania ambao “wamekumbusha kubwa Redio, televisheni na magazeti vinaweza kuwafikia mamilioni ya watu ambao mtandao wa inteneti bado ni ndoto au hawana fursa ya kuupata.”