Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwajibikaji ndio msingi wa upatanisho Myanmar:Burgener

Waislamu wa kabila la Rohingya kutoka Myanmar wakiwa katika msafara kuelekea Bangladesh. Wanakimbia nyumbani kwa sababu ya ukatili dhidi yao ambao UN inasema unaweza kuwa uhalifu wa kivita.
Hali ndani ya kambi ni mbaya sembuse Rakhine? Wahoji warohingya
Waislamu wa kabila la Rohingya kutoka Myanmar wakiwa katika msafara kuelekea Bangladesh. Wanakimbia nyumbani kwa sababu ya ukatili dhidi yao ambao UN inasema unaweza kuwa uhalifu wa kivita.

Uwajibikaji ndio msingi wa upatanisho Myanmar:Burgener

Wahamiaji na Wakimbizi

Uwajibikaji na majadiliano jumuishi ni mihimili miwli muhimu katika maridhiano ya kitaifa nchini Myanmar, amesema mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Schaner Burgener katika taarifa yake iliyotolewa Jumamosi.

Mwakilishi huyo ameongeza kwamba usakaji wa ukweli katika zahma ya Myanmar ni hatua ya kwanza katika kuelekea uwajibikaji.

Bi. Schrager amekuwa ziarani Myanmar ambako amekuwa na mazungumzo na viongpozi mbalimbali wa serikali na kijeshi, makundi ya kikabila yeney silaha, viongozi wa kidini wa kikanda na kitaifa, asasi za kiraia, mashirika yasiyo ya kiserikali NGO’s, mashirika ya Umoja wa Mataifa, jumuiya ya wanadiplomasia na kansela Aung San Suu Kyi.

Zaidi ya nusu ya wakimbizi wa kabila la rohingya huko Cox's Bazar nchini Bangldesh ni wanawake na wasichana ambao ni makundi yanayopatiwa kipaumbele zaidi na UNFPA  katika usaidizi wa kibinadamu
UNFPA Bangladesh/Naymuzzaman Prince
Zaidi ya nusu ya wakimbizi wa kabila la rohingya huko Cox's Bazar nchini Bangldesh ni wanawake na wasichana ambao ni makundi yanayopatiwa kipaumbele zaidi na UNFPA katika usaidizi wa kibinadamu

Katika jimbo la Rakhine na Kachin, Bi. Burgener amejaadiliana na raia na uongozi wa kijeshi lakini pia kuzungumza ana kwa ana na walioathirika na machafuko hususan wanawake. Na alipata fursa ya kutemebelea kambi kadhaa na maeneo walikohamishiwa wakimbizi wa ndani ili kujionea hatua zilizopigwa tangu alipozuru nchini hiyo kwa mara ya kwanza mwezi Juni 2018.

Takriban raia milioni moja wa kabila la Rohingya wanaishi makambini katika upande wa pili wa mpaka kwenye jimbo la Cox’s Bazar nchini Bangladesh baada ya kulazimika kukimbia makwao Kaskazini mwa Myanmar mwezi Agosti mwaka jana.


Ili kuhakikisha wakimbizi hao na watu wengine wanaweza kurejea nyumbani , haki zao za binadamu lazima ziheshimiwe amesema Bi. Burgener, kuanzia fursa sawa ya elimu na afya, na uhuru wa kutembea akiongeza kuwa “Ni lazima waweze kuishi kwa usalama , hii itakuwa ni kichocheo bora cha wakimbizi walioko Bangladesh kurejea nyumbani, waitambua kwamba Umoja wa Mataifa na wadau wake wapo katika maeneo wanayorejea kutawapa wakimbizi hao hali ya kujiamini na kuwa na Imani na mchakato mzima.”

Bi. Burgener pia amesisitiza haja ya uwekezaji wa ndani na wa kimataifa katika ukanda huo ambao ni moja ya maeneo masikini kabisa ya Myanmar ambayo yanahitaji haraka maendeleo jumuishi.

Katika jimbo la Kachine mwakilishi huyo amekutana na wakazi wa kambi ya wakimbizi wa ndani eneo la Myitkyina ambapo baadhi ya wakimbizi hao wamekuwepo tangu 2011 bila matumaini ya ajira au matumaini ya kurejea nyumbani kwa sababu ya mabomu ya kutegwa ardhini na ukosefu wa usalama na ametambua changamoto inayoongezeka ya kutopata fursa za masuala ya kibinadamu kama huduma za afya na misaada.

Wakina mama wakimbizi wa kabila la warohingya wakiwa na watoto wao wakisubiri watoto wao wachunguzwe katika kituo cha tiba huko Cox's Bazar nchini Bangladesh
UNICEF/Bashir Ahmed Sujan
Wakina mama wakimbizi wa kabila la warohingya wakiwa na watoto wao wakisubiri watoto wao wachunguzwe katika kituo cha tiba huko Cox's Bazar nchini Bangladesh

Akizungumzia wasiwasi wake kuhusu kupamba moto kwa mapigano katika eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo Bi.Burgener amerejerea pendekezo lake na kuwa kama daraja baina ya serikali ya Myanmar na makundi ya kikabila yenye silaha ili kuchapuza mchakato wa amani.

Ameichagiza serikali ya Myanmar kuchukua hatua za kutovumilia ubaguzi , na kusema anajikita katika kufanya kampeni dhidi ya hatua hiyo na kuendeleza juhudi zake katika kuimarisha uhusiano baina ya Myanmar na jumuiya ya kimataifa katika kuelekea kuwa na taifa linalovumiliana zaidi, la kidemokrasia na jamii jumuishi inatotambua mgawanyiko wa makundi mbalimbali ni amana.