Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa AU na UN ni ishara ya kupatiwa kipaumbele bara la Afrika

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Antonio Guterres ( wanne kushoto) akihutubia kikao cha ngazi ya juu kuhusu mchango wa ushirika kati ya UN na AU.
UN Photo/Loey Felipe
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Antonio Guterres ( wanne kushoto) akihutubia kikao cha ngazi ya juu kuhusu mchango wa ushirika kati ya UN na AU.

Mkutano wa AU na UN ni ishara ya kupatiwa kipaumbele bara la Afrika

Amani na Usalama

Mkutano wa kuimarisha  ubia kati ya Umoja wa Mataifa, UN na Muungano wa Afrika, AU ukitamatishwa hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, Uganda imesema fursa hii ni ishara ya kuendelea kupatia umuhimu mawazo ya Afrika katika chombo hicho chenye wanachama 193.

Akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kando ya mkutano huo, Naibu Mwakilishi wa kudumu wa Uganda kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Philip Odida amesema..

“Tumefurahi kuangalia kwamba sisi Afrika sasa  wameanza(kututambua) kutuangalia kama watu ambao wana mawazo yetu (kama ) Afrika nzima.Na hiyo ni kitu muhimu maanake hatutaki kutegemea assistance(msaada) kutoka nchi zingine mbalimbali(nje ya Afrika).

Amezungumzia pia fursa ya kujadiliana kuhusu kuimarisha usalama akisema..

 “Kwa vile bila usalama hauwezi kuende(lea). Sisi Uganda tunashirikiana na nchi zingine jirani,… (kuhusu suala la usalama)…tunaongea na neighbours; DRC, South Sudan na Somalia kwa vile tukiwa pamoja tunaimarisha mambo ya usalama,”