Ubia wa AU na UN waangaziwa New York

17 Oktoba 2018

Mkutano wenye lengo la kutathmini na kuchagiza ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika, AU unaanza leo katika makao ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani.

Mkutano huo wa siku mbili pamoja na kuangazia masuala hayo utajadili jinsi ya kubadili maneo kuwa vitendo hususan katika masuala ya amani na usalama duniani pamoja na kusaidia nchi za ukanda wa Sahel barani Afrika.

Miongoni mwa washiriki wa mkutano huu ambao awali ulitambulika kuwa sehemu ya wiki ya Afrika, ni Balozi Modest Mero, mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa ambaye tumemuuliza kwa kina wataangazia masuala yapi..

(Sauti ya Balozi Modest Mero)

Na kuhusu matarajio yao mwishoni mwa mkutano huu Balozi Mero anasema…

(Sauti ya Balozi Modest Mero)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter