Kundi la wapiganaji la CJTF lawaachia watoto 833 kaskazini mashariki mwa Nigeria.

12 Oktoba 2018

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, limekaribisha kitendo cha kundi la wapiganaji la Civilian Joint Task Force (CJTF) mjini Maiduguri, kaskazini mashariki mwa Nigeria, kuwaachilia huru watoto 833 ikiwa ni sehemu ya ahadi yake ya kuacha kuwatumia watoto katika mapigano.

Kupitia taarifa yake iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi na Maiduguri Nigeria, UNICEF imesema hii ni mara ya kwanza watoto kuachiwa kutoka CJTF tangu mwaka 2017 wakati kundi lilipotia saini  mpango kazi wa kuweka mikakati ya kuacha na kuzuia kuwatumia watoto kufuatiwa kuwa kundi hilo kutajwa katika tripoti ya mwaka ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu ya masuala watoto na matumizi ya watoto katika mapigano.

Pernille Ironside, ambaye ni Naibu mwakilishi wa UNICEF nchini Nigeria amesema kuachiliwa kwa watoto hawa kunaonyesha uwajibikaji au kujitolea katika kutekeleza vifungu vya mpango kazi na kutekeleza sheria za kimataifa za utu, haki za binadamu na pia sheria nyingine za kikanda na kitaifa ili kulinda haki za watoto.

Bi. Ironside ambaye pia ni  mwenyekiti mwenza wa kikosi kazi cha Umoja wa Mataifa nchini humo kinachofuatilia na kuripoti kuhusina na ukiukwaji wa haki za watoto amesema “hii ni hatua kubwa katika kuelekea kumaliza kuchukua watoto na kuwatumia katika vita lakini watoto wengi zaidi bado wanasalia katika makundi mengine ya wapiganaji katika nafasi ya upiganaji au katika majukumu ya usaidizi.”

Hadi kufikia hii leo, jumla ya watoto 1,469 kati yao wavulana 1,175 na wasichana 294 waliohusishwa na kundi hilo la wapiganaji, wameshatambuliwa jiji Maiduguri.

Tangu mwaka 2017, UNICEF imewasaidia kijamii na kiuchumi watoto ambao 8,700 ambao wameachiwa kutoka kwenye makundi ya wapiganaji. UNICEF pia imesaidia kuzitafuta familia zao, kuwarejesha katika jamii zao na kuwapa msaada wa kisaikolojia, elimu, mafunzo ya ufundi na fursa nyingine za kuboresha maisha yao.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter