Guterres atuma rambirambi kufuatia vifo nchini Nigeria

11 Oktoba 2018

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameeleza masikitiko yake makubwa juu ya ripoti za vifo vya watu 200 huko Nigeria vilivyosababishwa na mafuriko ambapo wengine 1,300 wamejeruhiwa.

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imesema kuwa watu wengine takribani milioni mbili wameathiriwa na mafuriko hayo yaliyokana na mvua kubwa zilizonyesha na kusababisha kufurika kwa mito Niger na Benue nchini Nigeria.

Habari zinasema mafuriko hayo yamesababisha wakimbizi wa ndani zaidi ya 500,000 na wengine zaidi ya 350,000 wanahitaji haraka misaada ya kibinadamu.

 

Mama na mwanae wakijaribu kujiokoa kwenye mafuriko yaliyokumba jimbo la Niger nchini Nigeria. Mafuriko yanatokana na mvua zinazonyesha jimboni humo tangu katikati ya mwezi Julai mwaka huu.
OCHA/UNDAC
Mama na mwanae wakijaribu kujiokoa kwenye mafuriko yaliyokumba jimbo la Niger nchini Nigeria. Mafuriko yanatokana na mvua zinazonyesha jimboni humo tangu katikati ya mwezi Julai mwaka huu.

Bwana Guterres ametuma salamu za rambirambi kwa wafiwa na serikali ya Nigeria pamoja na wananchi wake na kuwatakia ahueni ya haraka majeruhi.

Katibu Mkuu ameeleza mshikamamo wa Umoja wa Mataifa na Nigeria wakati  huu wa kipindi kigumu na kwamba Umoja wa Mataifa uko tayari kusaidia kwa kadri utakavyohitajika kufanya hivyo.

 

 

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter