Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO na AU zaunganisha nguvu kupambana na changamoto za afya barani Afrika.

Hii ni 06 June 2018 WHO na CDC walipokutana kujadili mlipuko wa Ebola DRC.
WHO/Lindsay Mackenzie
Hii ni 06 June 2018 WHO na CDC walipokutana kujadili mlipuko wa Ebola DRC.

WHO na AU zaunganisha nguvu kupambana na changamoto za afya barani Afrika.

Afya

Taarifa iliyotolewa leo mjini Brazzaville nchini Congo na Shirika la afya duniani WHO, imeeleza kuwa WHO na kamisheni ya muungano wa Afrika kupitia kituo chake cha kudhibiti na kuzuia magonjwa Afrika CDC wanaimarisha ushirikiano wao kwa kuungana kupambana na changamoto za kiafya zinazolikabili bara la Afrika.

Katika mkutano uliofanyika mjini Brazzaville Jamuhuri ya Congo, mashirika hayo mawili yamekubaliana kushikamana kufanya kazi kupitia kikosi kazi cha pamoja.

“Afya ya jamii inakabiliwa na changamoto kubwa kote barani Afrika na kwa kuunganisha nguvu zetu WHO na CDC tunaweza kuzisaidia nchi wanachama katika kuokoa maisha” amesema Dkt. Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika.

Mpango kazi wa awali unaonesha maeneo muhimu ambayo mashirikia haya yatashirikiana kuwa ni-msisitizo katika dharura, utayari, na usalama wa afya katika suala zima la kuimarisha mifumo ya afya.

Naye Amira Elfadil kamishina wa AU upande wa masuala ya kijamii amesema “Kuimarisha mifumo ya afya na kuelekea katika huduma ya afya kwa watu wote zinabaki kuwa vipaumbele vya juu kwa mataifa ya Afrika,”

WHO na kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa cha Afrika pia wamekubaliana kutengeneza mpango wa pamoja wa mwaka 2019-2020 ambao unaeleza kwa kina ni kwa namna gani mashirika haya mawili yataungana katika kutekeleza vipaumbele hivyo katika kaanda ya Afrika.