Matatizo ya afya ya akili ni changamoto kubwa kwa vijana na jamii:WHO

Nusu ya magonjwa yote ya akili duniani yanaaza katika umri wa miaka 14 na mengi ya hayabainiki wala kutibiwa, suala linaloweka mustakabali wa vijana wengi njia panda, limesema shirika la afya duniani WHO.
Katika tarifa ya siku ya afya ya akili duniani ambayo kila mwaka huadhimishwa Oktoba 10, WHO inasema mzigo wa matatizo ya akili miongoni mwa vijana barubaru unasababisha mambo makubwa matatu ambayo ni msongo wa mawazo , kujiua ikiwa ni sababu inayoshika nafasi ya pili kwa vifo vya vijana kati ya umri wa mika 15-19 na tatizo linaloongoza ni matumizi mabaya ya pombe na mihadarati , na kufanya matatizo ya akili kuwa moja ya changamoto kubwa kwa nchi nyingi duniani na huchangia kuwaweka vijana kwenye hatari kama ya kufanya ngono isiyo salama, na hata uendeshaji mbovu wa magari unaosababisha vifo vya vijana wengi.
Hi indio sababu kauli mbiu ya mwaka huu imejikita katika afya ya akili ya vijana. Dkt. Joyce Nato meneja wa WHO nchini Kenya kitengo cha magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo afya ya akili anafafanua sababu zinazochangia
(SAUTI YA DKT JOYCE NATO)
Na nini WHO inakifanya kuzisaidia nchi kukabiliana na changamoto hii
(SAUTI YA DR JOYCE NATO )
Athari za kutoshughulikia matatizo ya afya ya akili kwa vijana ni kubwa kwa mujibu wa WHO na mara nyingi zinaendelea hadi ukubwani na kuwakosesha fursa ya kushamiri katika maisha yao.
Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake wa siku hii amesisitiza kwamba ni muhimu serikali zikawekeza na kuhusisha sekra za afya, elimu na jamii katika kudhibiti janga hili ili kuhakikisha ajenda ya 2030 ya maendeleo haimuachi yeyote nyumba ikiwemo vijana wenye matatizo ya akili ambao hunyanyapaliwa na kukosa msaada wakati mwingine.