Tunaomba dola 66 milioni ili kuhudumia wakimbizi wa Rohingya:WFP

9 Oktoba 2018

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP linahitaji dola milioni 66 hadi mwezi Machi mwakani ili liweze kuendelea na usambazaji wa chakula kwa wakimbizi wa kabila la rohingya walioko ukimbizini nchini Bangladeshi.

Msemaji wa WFP mjini Geneva, Uswisi Herve Verhoosel   amewaambia waandishi habari hii leo kuwa fedha hizo zitaendeleza usambazaji wa mahitaji ambayo tayari wanawapatia wakimbizi hao kutoka Myanmar, akisema huko Cox Bazar peke yake wanatoa msaada wa chakula kwa zaidi ya wakimbizi 800,000 kila mwaka.

Bwana Verhoosel amezungumzia msaada wa dola milioni 22 kutoka Uingereza akisema.."Mchango mpya wa Uingereza wa dola milioni 22 utachangia katika shughuli mbalimbali za WFP. Hii ni pamoja na msaada wa chakula  kwa wakimbizi zaidi ya 680,000, vocha za ununuzi wa chakula kwa wakimbizi 250,000 pamoja na msaada muhimu wa lishe unaohitajika.”

 

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter