Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mauaji ya wanahabari wanawake yamefurutu ada:UNESCO

Waandishi habari wakiwa UN
UN Photo/Cia Pak
Waandishi habari wakiwa UN

Mauaji ya wanahabari wanawake yamefurutu ada:UNESCO

Wanawake

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO amelaani vikali mauaji ya kikatili ya Victoria Marinova , muandishi wa habari wa televisheni ambaye maiti yake ilikutwa mjini Ruse Bulgaria Oktoba 6 ikiwa na dalili za kuteswa kufanyiwa ukatili wa kingono.

Audrey Azoulay amesema “mashambulizi dhidi ya waandishi wa habari yanasigina haki za msingi za binadamu za uhuru wa kujieleza na vipengee vyake, uhuru wa habari, na uhuru wa kupata tarifa. Zaidi ya hapo matumizi ya ukatili wa kingozno na ukatili mwingine kumnyamazisha mwanahabari mwanamke ni ukiukwaji wau tu na haki za msingi za kila mwanamke.”

Azoulay ameitaka mamlaka kufanya uchunguzi wa kina dhidi ya uhalifu huu na kuwafikisha mbele ya sheria wahusika. Akiongoza kuwa hii ni muhimu katika kutetea uhuru wa kujieleza na uhuru wa habari nchini Bulgaria lakini pia ni muhimu kuhakikisha usalama, ut una uhuru wa wanawake.

Ameongeza kuwa “Zaidi ya hapo nina hofu kubwa kuhusu kuongezeka kwa idadi ya wanawake walio kwenye vyombo vya habari wanaoshambuliwa. Hii inahitaji kuongeza juhudi za wajibu wetu katika kushughulikia vitisho maalumu dhidi ya usalama wa waandishi wa habari wanawake.”

Victoria Marinova alikuwa mtangazaji wa kipindi cha habari za televisión  kilichojulikana kama “Detector” katika kituo binafsi tcha televisheni cha TVN.

Mwaka 2017 UNESCO iliorodhesha idadi kuwa ya waandishi wa habari wanawake waliouawa tangu mwaka 2006. Idadi ya wanahabari wanawake waliouawa mwaka jana iliongezeka hadi asilimia 14 kutoka asilimia 4 mwaka 2012. Mwaka jana waandishi wanne kati ya saba waliouawa Ulaya walikuwa wanawake.