Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uganda inajitahidi kudhibiti TB- Waziri Opendi

Chanjo ya BCG ambayo hutumiwa dhidi ya Kifua Kikuu ikiwa inaandaliwa katika kituo cha afya Bougouni, Mali 2018.
© UNICEF/Ilvy Njiokiktjien
Chanjo ya BCG ambayo hutumiwa dhidi ya Kifua Kikuu ikiwa inaandaliwa katika kituo cha afya Bougouni, Mali 2018.

Uganda inajitahidi kudhibiti TB- Waziri Opendi

Afya

Serikali ya Uganda imeanzisha kampeni ya kuhamasisha taifa zima kuhusu ugonjwa wa Kifua Kikuu, TB, ili kuongeza uelew wa ugonjwa huo hatari.

Waziri ya Afya nchini Uganda inasema kila mwaka watu 87,000 wanaambukizwa Kifua Kikuu nchini humo ambapo Waziri wa nchi anayehusika na masuala ya afya Sarah Opendi akihojiwa na idhaa kwa njia ya simu amesema..ugonjwa huo unawathiri watu wengini nchini humo

Waziri Opendi amesema uchunguzi uliofanywa nchini humo mwa 2017 ulionyesha kuwa maamabukizi ya TB kila mwaka ni watu elfu 87 na wala sio waliofikiria mwanzo wa Elfu 4.

Waziri Opendi akataja sababu ya idadi kuwa ya juu.

Moja ni kwamba watu hasa sehemu za vijijini wanadhani kuwa wamerogwa.