Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM Tanzania na harakati za kudhibiti usafirishaji haramu wa binadamu

Wahamiaji wakiwa kando mwa bahari mjini Lesbos, Ugiriki.
IOM/Amanda Nero
Wahamiaji wakiwa kando mwa bahari mjini Lesbos, Ugiriki.

IOM Tanzania na harakati za kudhibiti usafirishaji haramu wa binadamu

Haki za binadamu

Usafirishaji haramu wa binadamu ni suala ambalo bado linasumbua mataifa mengi duniani ikiwemo Tanzania, ambapo nchi zinapoteza rasilimali watu na pia watu hujikuta katika matatizo mbalimbali huko wanakopelekwa baada ya kulaghaiwa.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM, limekuwa katika jitihada za kuwaokoa watu na majanga haya ambapo katika kufahamu nafasi ya Umoja wa Mataifa katika vita hivyo, Stella Vuzo wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC huko Dar es salaam Tanzania amezungumza na Ena Lutengano afisa kutoka kitengo kinachoshughulika na masuala ya usafirishaji haramu wa watu, IOM, Tanzania.