Tafadhali Iran acheni hukumu ya kifo kwa watoto – Bachelet

5 Oktoba 2018

Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet hii leo mjini Geneva, Uswisi amelaani mauaji ya Zeinab Sekaanvand Lokran nchini Iran.

Kwa muijbu wa taarifa ya ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCRH, Bi Sekaanvand alishitakiwa kwa kumuua mume wake mwaka 2012 wakati alipokuwa binti wa miaka 17 lakini madai yake ilikuwa ni kwamba alilazimishwa kukubali na pia dai lake la kuwa kwa muda amekuwa muathirika wa manyanyaso ya nyumbani halikukuchunguzwa wakati wa hukumu.

“Ukosekanaji wa haki katika kesi ya Zeinab Sekaanvand Lokran ni jambo la kuumiza moyo” Bachelet amesema akiongeza kuwa,  “swali zito hapa liko katika hukumu yake inaonekana haikuzungumzwa kwa kina kabla hajanyongwa. Suala la muhimu hapa ni kuwa alikuwa na umri mdogo wakati kosa lilipotendeka na sheria ya kimataifa kwa uwazi inazuia kuwaua watenda makossa watoto”

“Iran inalazimika kufuata makubaliano ya kimataifa ya kulinda haki za mtoto na waache matumizi ya hukumu ya kifo kwa watenda makossa wa umri mdogo” ameongeza Bachelet.

OHCHR inasema pamoja na rufaa kadhaa zilizowasilishwa na wataalamu maalumu wa umoja wa mataifa na pia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa tangu kuhukumiwa kwake mwaka 2014, Sekaanvand amenyongwa mwezi huu Oktoba 2, 2018.

Familia yake ilipewa taarifa taarifa siku moja tu kabla ya kunyongwa ili waweze kumtembelea kwa mara ya mwisho.

Kukamatwa kwake na kesi yake yake vyote viliripotiwa kugubikwa na ukiukwaji mwingi wa taratibu za kisheria ikiwamo kupigwa na maafisa wa polisi wakati wa kukamatwa, na pia hakupewa nafasi ya kuwasiliana na mwanasheria hadi waakati wa mwisho wa hukumu wakati alipokana maelezo yake ya kwanza ya kukiri.

Ofisi hiyo ya  haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema watoto wengine wengi waliohukumiwa, inaripotiwa wanasubiri kutekelezwa kwa hukumu yao ya kifo nchini Iran, nchi ambayo tayari mpaka sasa kwa mwaka huu tayari imewanyonga watoto watano. “Mara nyingi utekelezaji wa hukumu ukitekelezwa katika kipindi cha muda mfupi kiasi cha kutokuwepo kwa mwanya wa  upelelezi na uwazi,” imesema taarifa hiyo.

Ni kwa mantiki hiyo Bi. Bachelet amesisitiza kuwa ofisi yake ya haki za binadamu inapinga hukumu ya kifo katika kila namna kwa kuwa hakuna mahakama ambayo katika namna moja au nyingine duninai kote haifanyi makosa.

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud

Fuatilia Habari: Habari zilizopita za Mada Hii

Naibu mkurugenzi wa IAEA anazuru Iran

Naibu Mkurugenzi wa Shirika la IAEA, Olli HEINONEN, ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Usalama amewasili Teheran Alkhamisi, kwa ziara maalumu ya siku mbili. Anatarajiwa kuongoza mazungumzo na maofisa wa vyeo vya juu wa Iran wanaohusika na sera za matumizi ya amani ya nishati ya nyuklia.~