Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Anga za mbali ni jukwaa la kuiunganisha dunia:

Kimbunga Florence kama kinavyonekana kutoka kituo cha anga za mbali  cha kimataifa.
ESA/NASA–A. Gerst
Kimbunga Florence kama kinavyonekana kutoka kituo cha anga za mbali cha kimataifa.

Anga za mbali ni jukwaa la kuiunganisha dunia:

Utamaduni na Elimu

Mchango wa anga za mbali kwa mwanadamu ni mkubwa na anga hizo zimeelezwa na chama cha wiki ya anga za mbali (WSWA), kuwa ni daraja la kuiunganisha dunia. Kwa kutambua umuhimu na nchango huo kila mwaka kunafanyika maadhimisho ya wiki ya anga za mbali kote duniani yakiambatana na shughuli mbalimbali ikiwemo kuwachagiza wanafunzi kutumia anga , kuchagiza program, será na mashirika ya masuala ya anga za mbali.

Kwa mujibu wa Goran Nikolasevic mkurugenzi mtendaji wa Umoja wa Mataifa katika WSWA, kauli mbiu ya wiki ya mwaka huu ni “anga za mbali zinaunganisha Dunia” kauli iliyochagizwa na mkutano wa kimataifa wa UNISPACE+50 uliomalizika mwezi juni mwaka huu kwa dhamira ya kuchagiza ushirikiano wa kimataifa katika kutafiti na matumizi ya anga za mbali.

Naye Dennis Stone rais wa WSWA amesema  “Wiki ya anga la mbali iliidhinishwa kwa mara ya kwanza na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 1999. Tangu wakati huo tukio hilo limekua likifanyika kila mwakakwa maadhimisho makubwa ya masuala ya anga hapa duniani,”

Kupitia azimio namba 54/68 la tarehe 6 Disemba 1999, Baraza kuu la Umoja wa Mataifa  lilitangaza wiki ya anga za mbali ili kusherehekea  mchango wa sayansi ya anga na teknolojia katika kuboresha maisha ya binadamu.