Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu bilioni 2.3 duniani hawana vyoo, hii ni hatari- WHO

Watoto wa shule wakienda kujihifadhi chooni katika jitihada za kudumisha usafi. Picha na UM

Watu bilioni 2.3 duniani hawana vyoo, hii ni hatari- WHO

Afya

Lengo la kila mkazi wa dunia kuwa na huduma za kujisafi ikiwemo choo halitafikiwa iwapo serikali hazitafanya mabadiliko ya kina na kuwekeza fedha zaidi kwenye sekta hiyo, limeonya shirika la afya ulimwenguni, WHO hii leo.

Katika mwongozo wake wa kwanza kuhusu huduma za kujisafi na afya uliotolewa hii leo, WHO imesem watu bilioni 2.3 duniani kote hawana vyoo wakilazimika kujisaidia maeneo ya wazi.

Shirika  hilo linasema idadi hiyo ni miongoni mwa watu bilioni 4.5 duniani kote wasio na huduma za kujisafi ikiwemo vyoo vyao kuunganishwa na mabomba ya kuondoa maji taka au mabwawa ya kusafisha maji hayo.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Soumya Swaminathan amesema huduma za kujisafi ni za  msingi kwa afya ya binadamu na maendeleo yake hivyo ni vyema serikali kufuatia mwongozo huo wa shirika lake.

“Kwa hila dola moja inayowekezwa katika huduma za kujisafi, kuna faida mara sita ikiwemo kupungua kwa gharama za afya, kuongezeka kwa tija kwenye uzalishaji na kupungua kwa kuzaliwa kwa watoto njiti,” amesema Dkt. Swaminathan.

Mwongozo huo una mapendekezo manne ambayo ni mosi, “ kuhakikisha jamii nzima ina vyoo ambamo kwavyo kinyesi kinadhibitiwa, pili mfumo mzima ukaguliwe uhakikishe kinyesi hakiwezi kuwa sehemu ya wazi, tatu mifumo ya kujisafi ijumuishwe katika mipango ya sera ya serikali za mitaa na kuhakikisha ni endelevu na nne fedha zaidi ziwekezwe kwenye sekta ya afya na sekta hiyo iwe na uratibu wa kina katika mipango ya kulinda afya ya umma.”

WHO imetaja baadhi ya  nchi ambazo tayari zimechukua hatua ili kuondokana na ukosefu wa huduma za vyoo na kujisai na moja wapo ni India ambayo imeelezwa kuwa chini ya mpango wa India Safi imeibua changamoto ya kutokomeza tabia ya watu kujisaidia maeneo ya wazi.

Nchini  nyingine ni Senegal ambayo inaongoza barani Afrika kwa kutambua dhimay a vyoo na mashimo ya majitaka katika kuhakikisha huduma bora za kujisafi kwa wote.

“Serikali hivi sasa kwa kushjrikiana na sekta binafsi inapatia jamii mbinu bunifu za kuwa na mashimo ya majitaka ambayo majitaka yanatolewa na kuwekewa dawa kwa gharama nafuu.