Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana mamlakani leo, ni wazee kesho! Pangeni mustakabali mnaotaka-Mtaalamu

Mzee Haron Jumma Bahar mwenye umri wa miaka 70 ambaye alikimbia kijiji cha Kobe akiwa karibu na kituo cha UNAMID kijijini Korma, Kaskazini mwa Darfur.
UNAMID/Owies Elfaki
Mzee Haron Jumma Bahar mwenye umri wa miaka 70 ambaye alikimbia kijiji cha Kobe akiwa karibu na kituo cha UNAMID kijijini Korma, Kaskazini mwa Darfur.

Vijana mamlakani leo, ni wazee kesho! Pangeni mustakabali mnaotaka-Mtaalamu

Haki za binadamu

Wakati kukishuhudiwa mabadiliko ya hali ya jamii, mchango wa wazee katika kuchagiza haki za binadamu ni muhimu sasa kuliko wakati mwingine.

Hivyo ndivyo ulivyoanza ujumbe wa Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu kwa wazee Rosa Kornfeld-Matte katika kuadhimisha siku ya wazee duniani hii leo Oktoba Mosi yenye kaulimbiu, “Kuwaenzi wanaharakati wazee wa haki za binadamu.”.

Mtaalamu huru huyo amesema, ni wajibu wetu kuhakikisha vizazi vijavyo- watoto wetu na wajukuu zetu- wakati wakizeeka watathaminiwe kwenye jamii.

Ameongeza kuwa vijana walioko katika mamlaka leo wanapaswa kufahamu fika kuwa watazeeka pia na ni wajibu wao kuweka mipango kwa mustakabali wanaotaka ili kuondokana na unyanyapaa na kunyimwa haki wakati wa uzee.

Bi.Kornfeld-Matte ametolea wito mataifa kuchukua hatua kulinda haki za kibinadamu za wazee.

Kwa sasa mataifa mbalimbali ikiwemo Kenya yameweka mikakati kwa ajili ya kuhakikisha haki za kundi hilo ikiwemo kutoa fedha kila mwezi kwa wazee na mipango mingine kama anavyofafanua Sicily Kariuki, waziri wa afya nchini humo..

(sauti ya Sicily Kariuki)