Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mamia wapoteza maisha na wengine kujeruhiwa kwenye tetemeko kubwa Indonesia:UN

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akitoa hotuba muhimu kuhusu mabadiliko ya tabia nchi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani 10 septemba 2018
UN/Eskinder Debebe
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akitoa hotuba muhimu kuhusu mabadiliko ya tabia nchi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani 10 septemba 2018

Mamia wapoteza maisha na wengine kujeruhiwa kwenye tetemeko kubwa Indonesia:UN

Msaada wa Kibinadamu

Kufuatia tetemeko la ardhi la ukubwa wa 7.5 vipimo vya richer katika jimbo la Sulawesi Katikati mwa Indonesia siku ya Ijumaa , Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ameshitushwa na janga hilo na idadi ya watu waliopoteza maisha na kujeruhiwa.

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake, idadi ya vifo na majeruhi inatarajiwa kuongezeka kufuatia tetemeko hilo la Ijumaa ambalo limesababisha uharibifu mkubwa ikiwemo miundombinu na maelfu ya majengo kuporomoka kwenye mji wa Palu katikati ya jimbo la Sulawezi.

Tweet URL

Duru za habari zinasema Tsunami iliyochochewa na tetemeko hilo imeambatana na mawimbi makubwa ya hadi mita tatu sawa na futi 10.

Taarifa za awali zinasema watu Zaidi ya 380 wamepoteza Maisha idadi ikitarajiwa kuongezeka ,shughuli za uokozi zinaendelea  lakini zimeelezwa kukabiliwa na changamoto ya kutokuwa na umeme na maporomoko ya udongo ambayo yameziba njia kuu iendayo Palu.

Katibu Mkuu ametuma salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza Maisha na kwa serikali ya Indonesia akiongeza kuwa Umoja wa Mataifa uko tayari kusaidia operesheni ya uokozi inayoongozwa na serikali na juhudi za misaada.

Na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa likiwemo shirika la afya duniani WHO yamesema yako tayari kujumuika kutoa msaada ukiwemo wa afya.