Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fursa ya utoaji mimba salama yahitajika kuokoa wanawake 47,000 kila mwaka:UN

Kuwalinda wanawake na wasichana kupitia utoaji mimba salama
Picha na WHO
Kuwalinda wanawake na wasichana kupitia utoaji mimba salama

Fursa ya utoaji mimba salama yahitajika kuokoa wanawake 47,000 kila mwaka:UN

Haki za binadamu

Nchi zote duniani zinapaswa kuchukua hatua sasa kutoharamisha utoaji miamba na kuhakikisha wanawake na wasichana wana haki ya kufanya maamuzi kuhusu hali ya ujauzito , wamesema wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa .

Katika tarifa yao ya pamoja ya kuadhimisha siku ya kimataifa ya utoaji miba salama, kundi la wataalamu hao wa Baraza la Haki l za Binadamu linalohusika na masuala ya ubaguzi dhidi ya wanawake katika vitendo na sheria , wamesema “ Utoaji mimba usio salama husababisha vifo 47,000 kila mwaka huku wanawake wengine milioni tano huathirika na aina fulani ya ulemavu wa muda .”

Kundi hilo limesisitiza kuwa uwezo wa mwanamke au msichana kufanya maamuzi yake mwenyewe kuhusu ujauzito “ni kitovu cha haki ya usawa , faragha na utu wa kimwili na kiakili na pia ni sharti la kuwafanya wafurahie haki zao na kuwa huru.”

Hivi sasa kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa inakadiriwa duniani kote wanawake milioni 225 wanakosa fursa ya kupata njia za kisasa za uzazi wa mpango hali inayochangia kupata mimba zisizotarajiwa. Kwa wasichana masuala kuanzia ujauzito na kujifungua ni miongoni mwa sababu kubwa za vifo vyao katika nchi zinazoendelea na wasichana wa umri wa chini ya miaka 15 wako hatarini mara tano zaidi ya wengine.

Wataalam hao wamesema “mifumo ya sheria kwa ajili ya utoaji mimba imewekwa ili kudhibiti maamuzi ya wanawake kwa kutumia sheria za uhalifu.”

Magu mwenye umri wa miaka 17 kutoka Hispania akisoma kitabu chake ni manusura wa ukatili wa kingono
Picha na UNICEF/Giuseppe Iperato
Magu mwenye umri wa miaka 17 kutoka Hispania akisoma kitabu chake ni manusura wa ukatili wa kingono

 

Takwimu za shirika la afya duniani WHO zinaonyesha kwamba kuharamisha utoaji mimba hakupunguzi idadi ya wanawake wanaoamua kusaka njia ya utoaji mimba, bali kunaweza kuongeza idadi ya watu ambao huishia kufanya utoaji mimba usio salama mitaani.

Na zaidi ya hapo “wanawake wengi hudhalilishwa kimwili na kwa maneno au kukataliwa huduma za dharura baada ya kutoa mimba hali ambayo ni njia nyingine ya adhabu ambayo inakiuka sheria na kimataifa na mara nyingi sera na sheria za kitaifa .”

Wataalamu wamekumbusha na kusisitiza kuwa serikali zina wajibu wa kuhakikisha kwamba wanawake na wasichana wanaotoa mimba wanatendewa haki na bila kuhukumiwa au kudhaniwa wamevunja sheria hususan katika wakati ambapo mimba imeharibika na kutoka kwa bahati mbaya.

Wameongeza kuwa wanatumai “hatua muhimu zitachukuliwa na zile ambazo tayari zimeshachukuliwa na baadhi ya nchi kurejesha haki ya afya ya uzazi kwa wanawake kwa kupitia kura za maoni, sheria na hatua za kikatiba ambazo wengine wanaweza kuziiga.”

Pia wametoa wito kwa hofu yao dhidi ya utoaji mimba usio salama kushughulikiwa kupitia afya ya jamii na humuma husika za afya na sheria za kiraia. Na hivyo ni muhimu kwa nchi kuonyesha dhamira ya kutokomeza ubaguzi dhidi ya wanawake katika sehria zao na kuboresha haki ya afya ya uzazi kwa wanawake na barubaru kwa mujibu wa viwango vya kimataifa vya haki za binadamu.