Hakuna mwanamke anayestahili kuuawa kwasababu ya jinsia yake:UN-EU

Umoja wa Mataifa na Muungano wa Ulaya EU leo wamezindua mkakati wa kukomesha mauaji dhidi ya wanawake na wasicha katika nchi tano za Amerika ya Kuisni kwa sababu tu ya jinsia yao, mkakati ujulikanao kama Spotlight.
Mkakati huu utakaoanza kutekelezwa nchini Argentina, El Salvador , Guatemala, Honduras na Mexico ni sehemu ya mkakati wa kimataifa uliozinduliwa mwaka 2017 utakaogharimu Euro milioni 500 kutoka EU zikilenga kuwekeza Asia, Afrika, Amerika ya Kusini , Pacific na Visiwa vya Caribbean kwa lengo la kubadilisha maisha ya wanawake na wasichana wanaokabiliwa na ukatili.
Akizungumza katika mkutano huo wa ngazi ya juu wakati kikao cha 73 cha Baraza Kuu la umoja wa Mataifa mjini New York Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed amesema wakati mwanamke au msichana anapouawa kwa sababu ya jinsia yake inadhihirisha hulka na mitazamo ya kijamii iliyopjengeka katika misingi ya kutokuwepo usawa na uwiano wa mamlaka vaina ya wanawake na wanaume
Ameongeza kuwa lengo la ushirika wa Umoja wa Mataifa na EU katika nchi hizo tano ni kuzisaidia kuendelea kukomesha mauaji ya wanawake na wasicha kwa misingi ya jinsia yao kwani zimeonyesha ujasiri wa kupambana na jinamizi hilo linalokatili maisha ya wanawake 12 kila siku Amerika Kusini
(SAUTI YA AMINA MOHAMMED)
“Amerika Kusini ni maskani ya nchi 14 kati ya 25 zilizo na kiwango kikubwa cha mauaji ya wanawake kwa sababu ya jinsia yao duniani huku asilimia 98 ya mauaji yanayohusiana na jinsia hayafunguliwli mashitaka.”
Ameongeza kuwa mkakati huu pia ni kuwakumbuka waathirika na familia zao wanaopigania haki za wapendwa wao kama Bi. Morena Herrera na pia Mariana Lima, aliyeuawa na mumewe afisa wa polisi mwaka 2010, na mama yake Irinea Buendía akupambana na mfumo wa sheria wa Mexico kwa miaka sita iliyoghubikwa na machungu mpaka muuaji wa mwaanye alipofikishwa mbele ya mkono wa sheria.
Mkakati wa Amerika Kuisni utagharimu Euro milioni 50 ambazo zimetangazwa leo kwa ajili ya kushughulikia masuala ya sheria, mapengo katika sera, kuimarisha taasisi, kuchagiza mtazamo wa usawa wa kijinsia, kutoa huduma kwa manusura, kuwhamisha waathirika na familia zao, kuandaa takwimu kuwezesha harakati za wanawake katika mataifa hayo matano.
Naye mwakilishi wa Muungano wa Ulaya Fredirica Mogherini amesema baada ya Amerika Kuisni uzinduzi utakaofuata utakuwa wa Afrika ukijikita katika kukomesha vitendo na aina zote za ukatili dhidi ya wanawake kwani
(SAUTI YA FEDERICA MOGHERINI)
“Tunaamini tunaweza kubadilisha sio tu Maisha ya wanawake bali pia ya wanaume na jamii nzima. Hebufikiria mwanawake wanauawa kwa sababu wamechagua kuwa huru, kufanya kazi wanaoipenda au kusoma wanachotaka , wanawake wanauuawa kwa sababu ya kuchagua nani wa kumpenda na nani wa kutompenda na wanauawa kwa sababu ya kuwa na malengo sawa na ya wanaume.”
Ameongeza kuwa hii si haki na ni lazima vitendo hivi vikome kwa nia ya kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu au SDG’s hususani lengo la usawa wa kijinsia.