Kisasi cha Mandela baada ya kutoka gerezani ni cha kuigwa- Dkt. Salim

24 Septemba 2018

Mwanadiplomasia nguli ambaye amewahi kufanya kazi na hayati Mzee Nelson Mandela azungumzia upekee aliokuwa nao mwendazake huyo ambaye leo anaenziwa na UN

Ikiwa leo Umoja wa Mataifa  unafanya tukio maalum kuhusu miaka 100 tangu kuzaliwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, hayati Nelson Mandela, mwanadiplomasia nguli nchini Tanzania na ambaye amewahi kuhudumu barani Afrika na Umoja wa Mataifa amemmwagia sifa hayati Mandela akisema kuwa alikuwa kiongozi shupavu ambaye kisasi chake baada ya kufungwa kilikuwa ni kuona watu wake wanaendelea.

Dkt. Salim Ahmed Salim ambaye alikuwa Rais wa mkutano wa 34 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na pia Katibu Mkuu wa uliokuwa Umoja wa nchi huru za Afrika amemweleza Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kuwa..

(Sauti ya Dkt. Salim Ahmed Salim)

Mwanadiplomasia akatoa ushauri wake kwa viongozi wa sasa kwa kuzingatia kile alichofanya Mandela..

(Sauti ya Dkt. Salim Ahmed Salim)

Mahojiano kamili ya Stella Vuzo na Dkt. Salim yanapatika hapa.

 

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter