Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa na Kofi Annan havitenganishiki- Guterres

Katibu Mkuu wa UN  António Guterres akigonga kengele ya amani katika tukio la kila mwaka lililofanyika makao makuu ya UN kuadhimisha siku ya amani duniani
UN /Mark Garten

Amani na Usalama

Leo ni siku ya amani duniani ambapo Umoja wa Mataifa ambapo Katibu Mkuu wa  Umoja huo ametaka watu wasikate tamaa katika kusongesha amani licha ya vikwazo vilivyopo.

Maadhimisho yamefanyika maeneo mbalimbali duniani ikiwemo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo hafla ilitanguliwa na muziki maalum uliporomoshwa na wacheza ala wenye umri kuanzia watoto wadogo hadi watu wazima, mbele ya kengele maalum ya amani.

Wageni ni pamoja na wajumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa akiwemo mcheza filamu mashuhuri Michael Douglas na waliongozwa na mwenyeji wao Katibu Mkuu Guterres.

Akihutubia hadhira hiyo Katibu Mkuu amesema “tunashuhudia mizozo ikiongezeka kila pahala duniani; tunaona jinsi mizozo na ugaidi vinavyohusiana; tunashuhudia jinsi ukosefu wa usalama unavyoshamiri na tunashuhudia jinsi watu wanapata machungu, lakini katu hatutokata tamaa.”

Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres (Kulia) katika maadhimisho ya siku ya amani duniani leo. Pichani ameungana na naibu wake Amina J. Moihamme (kushoto) na Rais wa Baraza Kuu la UN Maria Fernanda Espinosa (kati)
UN/Cia Pak

Siku ya amani ya Umoja wa  Mataifa ilianzishwa mwaka 1981 na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Miongo miwili baadaye, Baraza  Kuu kwa kauli moja lilitangaza siku hii ya amani duniani iwe siku ya kutovumilia ghasia na pia siku ya kusitisha mapigano ambapo Guterres amesema “tunafahamu kuwa tunawasihi wapiganaji waliojihami wasitishe mapigano na kuheshimu siku hii, tunafahamu wengi hawatoheshimu, lakini katu hatutokata tamaa.”

Baada ya hotuba hiyo, Katibu Mkuu aliambatana na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Maria Fernanda- Espinosa kugonga kengele ya amani iliyoko katika viwanja vya makao makuu  ya chombo hicho chenye wanachama 193.

Kengele hiyo ni zawadi iliyotolewa na Japan kwa Umoja wa Mataifa.