Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuboreshe mbinu za kubaini mauaji ya kimbari - Bachelet

Picha kwenye   katika makavazi ya mauaji ya kimbari ya Tuol Sleng ,Phnom Penh, Cambodia. Hapo ni mahali pa gereza maarufu wakati wa enzi ya Khmer rouge S-21
UN Photo/Mark Garten)
Picha kwenye katika makavazi ya mauaji ya kimbari ya Tuol Sleng ,Phnom Penh, Cambodia. Hapo ni mahali pa gereza maarufu wakati wa enzi ya Khmer rouge S-21

Tuboreshe mbinu za kubaini mauaji ya kimbari - Bachelet

Sheria na Kuzuia Uhalifu

Mauaji ya kimbari bado ni tishio kwa karne hii ya 21 na hivyo ni lazima tuchukue kila  hatua kuyaepusha.

Hayo yamesemwa na Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet wakati wa kikao cha 39 cha Baraza la haki za binadamu kilichokutana mahsusi hii leo mjini Geneva, Uswisi kuadhimisha miaka 70 ya mkataba wa kimataifa wa kuzuia na kuadhibu uhalifu utokanao na mauaji ya kimbari.

Bi. Bachelelet amesema miaka 70 tangu kupitishwa kwa mkataba huo bado kuna tishio hilo akigusia kile kinachoendelea huko Myanmar dhidi ya waislamu wa kabila la Rohingya.

“Jopo la Baraza hili lililokwenda kuchunguza ukweli kwenye jimbo la Rakhine nchini Myanmar limetoa ripoti ya kutisha ya kampeni inayoongozwa na  jeshi la nchi hiyo katika mauaji, ubakaji na mashambulizi dhidi ya warohingya kwenye jimbo la Mynmar,” amesema Bi. Bachelet na kuendelea.

Mkataba kuhusu mauaji ya kimbari ni muhimu leo kama ulivyokuwa Disemba 9 mwaka wa 1948, siku ulianza kuwa mkataba wa kwanza kuhusu haki za binadamu uliopitishwa na baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

 Hatua ya kuupasisha, ilifuatiwa na kuidhinishwa kwa tamko la haki za binadamu duniani.”

Kamishna huyo mkuu wa haki za binadamu amesema ni dhahiri kuwa viashiria vya mauaji ya kimbari vinakuwepo lakini, “moja ya changamoto kubwa iliyosalia, miaka 70 baada ya kupitishwa kwa mkataba huu ni kuboresha mbinu za kutambua na kuchukua hatua dhidi ya viashiria vya mauaji ya kimbari ikiwemo kauli za chuki iwe katika mazingira ya halisia au mitandao ya kijamii.”

Amekaribisha hatua ya wiki iliyopita ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC kusema kuwa ina mamlaka ya kuchunguza kufukuzwa kwa warohingya kutoka Myanmar akisisitiza ushirikiano na mahakama hiyo katika kuchukulia hatua kesi ambazo serikali zinasita kushtaki wahusika.

Amesema ni kwa mazingira kama hayo inaondoa shaka kuwa mkataba huo bado ni muhimu hii leo kama ilivyokubwa tarehe 9 disemba mwaka 1948 ulipopitishwa na na kuwa mkataba wa kwanza wa kimataifa kupitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kesho yake kufuatiwa na tamko la haki za binadamu.