Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baada ya WEDF2018 mjasiriamali mtanzania kuchagiza biashara ya nje.

Mavuno ya mpunga
Photo: FAO/Olivier Thuillier
Mavuno ya mpunga

Baada ya WEDF2018 mjasiriamali mtanzania kuchagiza biashara ya nje.

Ukuaji wa Kiuchumi

Wajasiriamali walioshiriki jukwaa la kimataifa la kuendeleza biashara ya nje, WEDF2018 nchini Zambia wamesema kilichobakia sasa baada ya kupata stadi na hamasa, ni kuhamasisha serikali zao kuondoa vikwazo wanavyokumbana navyo wakati wa kuuza bidhaa zao nje ya nchi.

Miongoni mwao ni Martin Silayo,  meneja  uzalishaji wa  kampuni  ya Union Service Stores kutoka Tanzania inayohusika na kuongeza thamani ya bidhaa ambaye akihojiwa na Stella Vuzo wa Umoja wa Mataifa ametoa mfano wa baadhi ya vikwazo.

Bwana Silayo ambaye kampuni yake ni mwanachama wa kituo cha biashara cha kimataifa, ITC waandaaji wa jukwaa hilo amesema anaporejea nyumbani atakalofanya akirejea nyumbani ili vijana wengi zaidi waungane na ITC.