Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko katika operesheni za ulinzi wa amani ni lazima:UN

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania walio kwenye kikosi maalum cha kujibu mashambulizi cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC.
MONUSCO Forces/FIB-TANZBATT
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania walio kwenye kikosi maalum cha kujibu mashambulizi cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC.

Mabadiliko katika operesheni za ulinzi wa amani ni lazima:UN

Amani na Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limefanya mjadala maalumu kuhusu mabadiliko katika operesheni za ulinzi wa amani na njia za kuongeza ufanisi katika operesheni hizo

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa mabadiliko katika operesheni hizo ni lazima kwani yatasaidia kuongeza ufanisi, kubana matumizi lakini pia kuhakikisha yanashughulikia changamoto zinazozikabili nchi wanachama wanaochangia vikosi vya kulinda amani wanapokuwa katika operesheni hizo.

Umesisitiza kwamba kuwawezesha walinda amani kwa kuhakikisha masuala kama vifaa, mafunzo na kutatua changamoto zingine zinazowakabili kutasaidia kutekeleza majukumu ipasavyo kwa mujibu wa maazimio ya Umoja wa Mataifa.

Meja Jenerali Alfred Fabian Kapinga ni mkuu wa operesheni na mafunzo wa jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ), moja ya nchi wachangiaji wa vikosi katika operesheni za ulinzi wa amani kwenye nchi mbalimbali, anaafiki mabadiliko ni muhimu na wameanza kuyafanyia kazi kwa kubadili mundo mfano huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ambako Tanzania inashirikiana na Afrika Kusini na Malawi kuunda kikosi maalumu cha kujibu mashambulizi kijulikanacho kama FIB. 

 MEJA JENERALI ALFRED FABIAN KAPINGA

Na kuhusu changamoto ikiwemo kupoteza walinda amani katika opereshini kama ilivyowatokea Watanzania huko Semuliki Mashariki mwa DRC amesema