Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanaoshambulia raia Afghanstan lazima wawajibishwe:UNAMA

Baada ya shambilizi la kigaidi nchini Afghanistan
UNAMA/Jawad Jalali (file)
Baada ya shambilizi la kigaidi nchini Afghanistan

Wanaoshambulia raia Afghanstan lazima wawajibishwe:UNAMA

Amani na Usalama

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan , (UNAMA) umeshutumu mfululizo wa mashambulizi ya mabomu hii leo katika jimbo la Nangarhar mashambulizi ambayo yameua takribani raia 21 na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa, na kusema unatiwa hofu na mashambulizi hayo ambayo yanawalenga raia na shule.

Wananchi wengi wamejeruhiwa katika wilaya ya Mohmandara jimboni Nangarhar wakati mshambuliaji wa kujitoa muhanga alipojilipua katikati ya umati ambao ulikusanyika kuandamana dhidi ya kamanda wa Polisi wa Afghanistan.

Nangarhar, na mji mkuu wake Jalalabad, hivi karibuni imeshuhudia mashambulizi mengi ya makusudi yanayotekelezwa na wapinzani wa Serikali hasa mashambulizi hayo yakiwalenga wananchi na vitu vingine vya kiraia, pia katika shule ambazo zimekuwa zikilengwa  na washambuliaji hao tangu mwezi Juni.

Katika kipindi cha dakika 15 leo Jumanne asubuhi, si chini ya shule tatu zilizoshambuliwa katika wilaya ya Bihsud jimboni Nangarhar na Jalalabad. Shule mbili za sekondari za wasichana zimezilipuliwa na mtoto mmoja wa kiume wa umri wa miaka 12 aliuawa huku watoto kadhaa walijeruhiwa , na mlipuko wa pili ulitokea wakati wahudumu wa misaada na wana familia walipokimbilia katika eneo la mlipuko wa kwanza.

Wanaume kadhaa ambao  walijeruhiwa katika mlipuko huo. Na mlipuko wa tatu ulitokea baada ya vilipuzi kutegeshwa karibu na shule na bomu la tatu lipatikana na kuteguliwa na wataaalamu wa vilipuzi. Watoto wamerejea shuleni siku za hivi karibuni baada ya likizo yao ya majira ya joto.

" Tadamichi Yamamoto, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini  Afghanistan amesema "Ninajihisi gadhabu kubwa kutokana na wimbi hili la hivi karibuni la mashambulizi ya makusudi dhidi ya raia. Huruma yetu iko pamoja na waathirika, familia na watu wa Afghanistan. Mabomu shuleni na mauaji ya watoto ni miongoni mwa vitendo vya ugaidi ambavyo vinakiuka sheria za kimataifa za kibinadamu. Ameongeza kuwa "Wapangaji wa matukio haya wanapaswa kukabiliana na mkono wa sheria."

UNAMA inazikumbusha pande zote katika mgogoro kuzingatia wajibu wao wa kulinda raia na kuwataka mara moja kuacha kuwalenga raia pamoja na miundombinu yao kama vile shule, na kufuata sheria za kimataifa za haki za kibinadamu.