Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hukumu ya kifo dhidi ya watu 75 Misri haikuzingatia haki:Bachelet

Waandamanaji waliojawa na hasira watupia polisi mawe mjini Cairo katika maadhimisho ya pili ya kuondolewa  mdrakani kwa Hosni Mubara mwaka 2011.
IRIN/Amr Emam
Waandamanaji waliojawa na hasira watupia polisi mawe mjini Cairo katika maadhimisho ya pili ya kuondolewa mdrakani kwa Hosni Mubara mwaka 2011.

Hukumu ya kifo dhidi ya watu 75 Misri haikuzingatia haki:Bachelet

Sheria na Kuzuia Uhalifu

Hatua ya mahakama moja nchini Misri ya kuthibitisha hukumu ya kifo kwa watu 75, haikufuata utaratibu unaostahili katika kusikiliza kesi na endapo hukumu hiyo itatekelezwa itakuwa ni ukiukwaji mkubwa wa haki.

Kauli hiyo imetolew leo na Kamishina mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet,na kuongeza kuwa hukumu hiyo iliyotolewa Jumamosi inamtoa wasiwsi mkubwa.

Ameongeza kuwa suala linguine linalokiuka haki ni hatua ya hatua ya Misri ya kuwahukumu watu wengi kwa mkupuo na sheria mpya  iliyopitishwa ambayo inawapa kinga maafisa wa vyombo vya dola  dhidi ya kushtakiwa kutokana na makosa ambayo huenda wameyatenda.

Hukumu hiyo ya kifo ilitangazwa vifo wakati wa hukumu ya pamoja iliyotolewa Julai mwaka huu ambapo watu 739 walihukumiwa kwa makossa mbalimbali kutokana na maandamano  ya Agosti mwaka   wa 2013 yaliyoongozwa na wafuasi wa kundi la Muslim Brotherhood ambayo yalizimwa na jmabavu ya jeshi la polisi..

Bi. Bachelet amesema, “ jinsi kesi ilivyoendeshwa katika  mahakama ya jinai mjini Cairo, imekosolewa vikali…na ni sahihi kufnya hivyo, watu 739 wameshtakiwa kwa mkupuo na hawakukubaliwa hata mmoja kuwakilishwa na mawakili mahakamani na wala hawakupewa fursa ya kujitetea.” 

 Ameongeza kuwa, “washukiwa hawakupewa haki ya kutoa ushahidi wao na pia upande wa mashtaka haukutoa  ushahidi wa kutosha kuweza kuthibitisha kweli wana hatia .Hivyo hukumu ya kifo kwa watu 75 iliyohakikishwa jana, endapo itatekelezwa itakuwa ni ukiukwaji mkubwa wa haki na sharia ambao haitowezekana kuugeuza.”

Bi Bachelet amesema ni matumaini yake kuwa mahakama ya rufaa ya Misri itatengua hukumu hiyo na kuhakikisha kuwa viwango vya kimataifa vya sheria vinafuatwa na pia vinaheshimiwa.

 

Jiji la Cairo Misri
Dominic Chavez/World Bank
Jiji la Cairo Misri

 

Kamatakamata ya jeshi dhidi ya maandamano ya kundi la Muslim Brotherhood katika maeneo ya Rabaa al-Adawiya, uwanja  wa Rabaa al-Adawiya na katka jukwa la Nahda mjini Cairo  tarehe 14 Agosti 2013, yanadaiwa kusababisha vifo vya watu 900 na wengi ni raia ambao hawakuwa na silaha. Mauaji yanadaiwa kufanywa na vikosi vya serikali ya Misri. Baadae serikali ilidai kuwa waandamanji wengi walikuwa wamebeba silaha na kuwa polisi kadhaa waliuawa.

Wakati huohuo Julai mwaka huu, bunge la Misri lilipitisha sheria inayowapa kinga askari dhidi ya makossa yaliyotokea kati ya Julai 3 2013, hadi siku ambayo jeshi lilipindua serikali ya rais Morsi na pia Januari 10 mwaka wa 2016.

Sheria hiyo inampa uwezo rais  kuwateuwa  askari kadhaa kuwa askari wa kikosi cha akiba na kuwapa kinga  na vile vile kumpa kinga ya kidiplomasia  waziri yeyote akiwa ofisini au akiwa ziarani nje ya nchi.